Sunday, April 6, 2014
Thursday, March 27, 2014
Taswira toka Lake Manyara National park
Eneo linalojulikana kama maji ya moto ambalo lipo pembezoni ya ziwa
Manyara (linaloonekana kwa mbali). Asikwambie mtu, haya maji ni ya moto
kweli kweli.. usiende kichwa kichwa kutest joto lake, unaweza ukaiona
safari ya porini chungu.
Mateja wakiwa wanapumzika mida ya mchana baada ya mihangaiko yao
Japo ni kama mweusi lakini wanaitwa Blue Monkey akiwa Manyara NP.
Shukran ya picha kwa mdau Aenea
TIGO NGORONGORO MARATHON
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tigo Ngorongoro Marathon kuchangisha fedha kwa ajili ya kukumbana na Malaria nchini
Dar es Salaam, 17 Machi 2014 – Mwaka wa saba wa ‘Tigo Ngorongoro Half Marathon’ iliyopewa kauli mbiu ya “Kimbia kuikabili Malaria” itafanyika Jumamosi ya 19 Aprili 2014 wilayani Karatu, jijini Arusha. Mbio hizo za kila mwaka inategemea kuwavutia wanariadha 3000 wa kitaifa na kimataifa, Tigo ilitangaza leo.
Tigo Ngorongoro Marathon kuchangisha fedha kwa ajili ya kukumbana na Malaria nchini
Dar es Salaam, 17 Machi 2014 – Mwaka wa saba wa ‘Tigo Ngorongoro Half Marathon’ iliyopewa kauli mbiu ya “Kimbia kuikabili Malaria” itafanyika Jumamosi ya 19 Aprili 2014 wilayani Karatu, jijini Arusha. Mbio hizo za kila mwaka inategemea kuwavutia wanariadha 3000 wa kitaifa na kimataifa, Tigo ilitangaza leo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja
Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha, alisema kwamba Tigo Ngorongoro
Marathon ni fursa ya kuhamasisha jamii kuhusu jinsi ugonjwa wa Malaria
unavyoathiri watu milioni 300 mpaka 500 duniani, asilimia 90 wakiwemo
barani Afrika.
“Malaria inaua zaidi watu milioni moja kila mwaka. Nchini Tanzania
mtu mmoja anafariki kwa ugonjwa wa malaria kila baada ya dakika 10. Mbio
za mwaka huu inahusisha pia harambee yakujenga kituo cha hospitali,”
alisema Wanyancha.
Mwaka wa 7 wa mbio hizi za Tigo Ngorongoro Half Marathon inaambatana
na maadhimisho ya Siku ya Malaria inayoadhimishwa tarehe 25 Aprili kila
mwaka. Tukio hilo, kutokana na maelezo ya Wanyancha inategemewa
kuzinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu kama
mgeni rasmi.
Tigo inashirikiana na moja ya makampuni ya utalii yanayoongoza nchini
kwa jina la Zara Tanzania Adventures, katika kuandaa mashindano haya,
ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kununua na kugawa neti za mbu,
pamoja na kununua dawa za malaria ambapo zitagawiwa mahospitalini
Arusha bure.
Fedha zitakazochangishwa pia mwaka huu zitatumika kukarabati vituo
vya afya vilivyopo pamoja na kujenga kituo kipya cha afya
kitakachoanzishwa Ngorongoro pamoja na shule ya awali katika vijiji
tofauti tofauti kwa gharama ya shilingi milioni 160 jumla, alisema
Wanyancha.
“Mbio za Tigo Ngorongoro half marathon sio tu burudani kwa watu watakaoshuhudia bali ni sehemu nzuri sana yenye kuhamasisha kuhusu namna ya kujikinga na kutibu ugonjwa wa malaria kwa jamii inayozunguka maeneo ya Monduli na Arusha kwa ujumla,” alisema.
Mbio hizi zinawapa fursa wanariadha kukimbia katika sehemu moja yenye
vivutio vya kipekee duniani, kutoka kivutio cha Ngorongoro mpaka jiji
la Karatu. Mbio za mwaka huu pia inahusisha mashindano ya makampuni ya
kilomita 5 kwa makampuni wenye nia yakuchangia katika harambee hiyo.
Kutokana na maelezo ya Mratibu wa Mbio hizo, Datus Joseph, kampuni zinazaodhamini mbio hizi katika ngazi za mashindano ya makampuni ni SBC Tanzania Ltd, CHUCHU, BG Tanzania, Hans Paul, Mberesero Lodge Tented Camps, Afrika-Safari, Orange gas na BIL
Kutokana na maelezo ya Mratibu wa Mbio hizo, Datus Joseph, kampuni zinazaodhamini mbio hizi katika ngazi za mashindano ya makampuni ni SBC Tanzania Ltd, CHUCHU, BG Tanzania, Hans Paul, Mberesero Lodge Tented Camps, Afrika-Safari, Orange gas na BIL
Ni Kundi la Makapela

ukikutana na kundi la swala na wote wa pembe, jua hilo ni kundi la swala makapela.


Mdau alishuhudia 'Live' hili windo la Wahadzabe
Ni Mdau Thomas wa HSK Safaris
ambaye alikuwa maeneo ya pembezoni mwa Ziwa Eyasi wanakoishi watu wa
kabila ya Wahadzabe. Siku hii waliongozana na wenyeji (Wahadzabe) kwenda
kwenye mawindo yao ya kujitafutia chochote. Kwa mujibu wa mdau Thom,
huyu jamaa alimdungua huyu ndege (Hondohondo) kwa mshale mmoja tu.
Shughuli nzima ilichukua kama dakika 10 hivi za kumnyatia na baada ya
mshale kuchomoka, hondohondo alianguka chini mzima mzima.
Kwa tulio mjini na maeneo yaliyopiga hatua, mshale unaweza onekana kama
zana duni lakini hawa Wahadzabe mshale ndio silaha yao kuu ya kuwindia
na inaelezwa ya kwamba wana shabaha ajabu. Kabila hili wao hula nyama
pamoja na matunda, majani au mizizi wanayookoteza porini. Hawalimi mazao
kama jamii nyingine. Nyama wanayokula huipata kwa mawindo kama hili
ambalo siku hii walimkaribisha Tom na wageni wake kulishuhudia. Ni
Kabila mojawapo ambalo linawavutia wageni wengi kuwatembelea ili
kushuhudia na kuona mfumo wao wa maisha kwa ukaribu. Wana mengi ambayo
yatakuacha mdomo wazi na usiweze kuamini kuwa kwenye karne hii ya
digitali kuna jamii zinaishi maisha kwa mfumo huu. Hawa ndugu zetu
wanalinda na kudumisha mila zao kwa miaka na miaka. Hata ukienda kwenye
mtandao Wikipedia (Bofya hapa)
na kusoma habari za kabila hili utakutana na vitu vingi. Baadhi ndio
kama hivi ambavyo mdau Thomas amekutana navyo hukoe Lake Eyasi wiki
chache zilizopita.Nyani na Ndegere wapo kwenye menu yao pia, na nimedokezwa na mdau kuwa endapo Nyani anakutana uso kwa uso na hawa jamaa wakiwa mawindoni, basi Nyani/Ndegere huanza kutoa milio ya ajabu hali ya kuashiria kupoteza matumaini. Wakikutana na Nyani hawamuachi na mshale ukitoka kwenye upinde basi subiri kusikia akidondoka chini muda mfupi baadae. Siku hii mdau Tom anasema kuwa kundi lao halikukutana na nyani wakati wa windo lao, badala yake jamaa wakawapa demo ya huyu Hondohondo kama anvyoonekana kwenye picha ya juu. Waliowatangulia siku moja kabla walipata bahati ya kushuhudia windo la Nyani na wanasema Nyani alitoa kilio cha ajabu sana baada tu ya kuwaona jamaa wakiwa karibu nae kwenye hali ya kumnyatia.
Napenda kusisitiza tena, Utalii sio wanyama na mapori tu. Jamii nazo zina mengi ya kuweza kutufundisha na kutuelimisha na hata kukuburidisha. Kama utalii wa Mbuga na Maporini unauogopa basi hata huu wa mila na desturi sambamba na mambo ya kale na kihistoria unaweza kukupa mawili matatu yakakufanya uifahamu Tanzania vyema na ukaielezea vizuri zaidi kwa wasioifahamu. Picha ya pili ni Wanajamii wa Kabila la Wahadzabe wakipumzika na kupata kazi na dawa kabla ya kuendelea na shughuli zao za kutafuta chochote wakiwa sambamba na wageni wao. Picha zote na Mdau Thomas wa HSK Safaris
Subscribe to:
Posts (Atom)






