Wanyama
kazi kijijini kama Punda hutumika sana katika kusafirisha Migo kutoka mashambani hadi sokopni au majumbani, wanyama hawa ambao wakati
mwingine hukokota matela ya mizigo hutumia barabara hivyo kulazimika
kufuata sheria za Usalama barabarani ili kulinda usalama wa wanyama hao
na waongozaji wake. Elimu ni muhimu kutolewa kwa watu mbalimbali wanao
waongoza wanyama hawa ili kuepusha kutokea ajali wawapo barabarani.
Taifa lipo katika maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama ambayo
inaadhimishwa Mkoani Iringa huku ikiwa na kauli mbiu ya Maadhimisho ya
mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA
SHERIA”.
Vijana na watoto wa Kitongoji cha Kinyenye, Kijiji cha Kipera wilaya
ya Mvomero mkaoni Morogoro wakishusha Matofali ya kuchoma
yaliyosafirishwa na Punda. Wanyama hawa wamekuwa msaada mkubwa wa
usafiri vijijini.
No comments:
Post a Comment