Kalambo
Falls ambayo ni maporomoko makubwa ya maji ya asili yanayochukua nafasi
ya pili kwa ukubwa barani Africa yakiwa na urefu wa mita
235 yanapatikana Mkoani Rukwa mpakani na nchi jirani ya Zambia ni
miongoni mwa vivutio vya asili nchini Tanzania vyenye hadhi ya kupigiwa
kura kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili nchini Tanzania na barani
Afrika kwa ujumla. Vivutio vya Tanzania vinavyoshindanishwa na vingine
tisa (9) barani Afrika katika nafasi ya maajabu saba barani Afrika ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Pigia
vivutio hivi vitatu na vingine vinne ikiwemo Kalambo Falls kupata
vivutio 7 vya maajabu ya asili nchini Tanzania na barani Afrika.
PIGA KURA YAKO KUPITIA HAPA http://sevennaturalwonders.org/tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya alipotembelea maporomoko hayo hivi karibuni.
Mbunge
Viti Maalum CCM Geita Vicky Kamata alipotembelea maporomoko hayo hivi
karibuni kwa ajili ya kupiga picha za kutangaza kivutio hicho na
vinginevyo vinavyopatikana katika Mikoa ya Rukwa, Katavi na Tanzania kwa
ujumla. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)
Kalambo Falls.
Habari na picha by John Bukuku
No comments:
Post a Comment