Taswira toka hifadhi ya taifa ya Mikumi kama zilivyonaswa na mdau Rajab toka Wildness Safaris Tanzania
hivi Karibuni. Ni picha za wanyama mbalimbali wakipata malisho yao ya
mwisho kabla jua kuzama na kuelekea sehemu zao za kuegeshea mbavu zao
Swala Tomi na Nyani hupenda kutembea pamoja hususan kwenye maeneo yenye
miti na vichaka. Hii ina manufaa kwa wanyama wa jamii zote mbili - Swala
na Nyani. Nyani anapokuwa juu anakuwa na uwezo wa kuonda mbali na kutoa
ishara kwa wengine kama hali ya usalama inaelekea kwenye dosari ktk
eneo waliopo. Hii itawasaidia Swala nao kuweza kuiona hatari ikiwa mbali
kabla haijawafikia. Na si hivyo tu, palipo na miti Mingi Nyani na
ngedere hutupa chini maganda ya matunda walayokula juu mtini. Hii nayo
huwa ni lishe kwa swala walio chini ambao kwa mazingira ya kawaida
wasingeweza kuyafuata matunda/maganda hayo juu mtini.
Sio serengeti tu, Hata mikumi Nyumbu wapo japo wao hawami kama wenzao wa kule Serengeti.
Ni Hali halisi ilivyo hivi sasa ktk hifadhi nyingi ukanda huu baada ya
kipindi kirefu cha jua kali. Taarifa za kuwepo kwa mvua maeneo
mbalimbali nchini zinaweza kuleta neema kwenye hifadhi zetu na
kubadilisha mandhari kuwa ile kijani ya Asilia.
Jioni njiani kurudi Camp site. Wageni wengi wanaotembelea Hifadhi ya
Mikumu hulala ktk hotel na camp sites zilizopo nje ya hifadhi ukiachia
wachache ambao hulala kwenye camp site uijulikanayo kama Vuma Hill
Tented camp site.
Poz kwa poz...
Shukran ya picha kwa Mdau Rajab na timu nzima ya Wildness Safaris Tanzania
No comments:
Post a Comment