Na: Geofrey Tengeneza
Waziri wa Maliasili na
Utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki anatarajiwa kuzindua mkakati wa
utangazaji utalii wa kimataifa tarehe 15/11/2012 katika hoteli ya Serena
hapa jijini Dar es salaam.
Mkakati huo unaotarajiwa kuwa
ndio dira ya kuitangaza Tanzania kama eneo la utalii duniani
umetengenezwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na
Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT) linajumuisha wadau mbali
mbali katika sekta ya utalii hapa nchini.
Hafla hiyo itakayofanyika kuanzia
saa 12.30 jioni itahudhuriwa pia na Naibu Waziri Maliasili na Utalii
Mh. Lazaro Nyalandu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi
Maimuna Tarishi, Naibu Katibu Mkuu Bibi Nuru Milao na viongozi wengine
kutoka Wizarani. Aidha viongozi wa Shirikisho la vyama vya utalii nchini
TCT na wadau wengine wa sekta ya utalii watahudhuria pia hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment