Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo akizungumza na Ujumbe wa
wandishi wa habari kutoka Misri huko Wizarani,wandishi hao walitembelea
maeneo kadhaa ya Kiutalii Zanzibar.
……………………………….
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar
Waziri
wa Habari,Utalii ,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk amesema kuwa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzíbar inakusudia kuifanya sekta ya utalii
kuongeza nafasi za ajira kwa wananchi wake ili kuinua kipato chao na
Taifa kwa ujumla.
Hayo
ameyasema leo huko Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo wakati
alipokutana na Waandishi wa Habari kuto nchini Misri waliofika Zanzíbar
kujionea shughuli mbalimbali za utalii zinavyofanywa na kuweza
kuitangaza Zanzíbar katika nchi ya Misri.
Amesema
hali hiyo itafikiwa kwa kuwepo misingi imara ya uwekezaji na kupokea
watalii wa daraja la juu ambao wana nafasi kubwa ya kuongeza ajira
katika maeneo ya mijini na vijijini ili kuondoa umasikini .
“unapolikuza
soko la utalii nikutangaza utalii hivyo ni matumaini yetu kuona tuna
pokea watalii wenye kipato ambao watatoa ajira zaidi katika nchi”
alisema Waziri Mbarouk.
Aidha
Waziri huyo alisema kuwa suala hilo litafanikiwa kutokana na
kuimarishwa miundo mbinu ya uwekezaji,fukwe zilizo bora, hoteli za
kimataifa na mashirikiano mazuri yanayofanywa na wadau wa sekta hiyo
ikiwemo mashirika ya ndege ,watembezaji wageni na wawekezaji wa
mahoteli.
Alisema
hiyo ni nafasi ya kipekee kwani itaongeza nafasi za ajira kwa Wananchi
na kupelekea kukua kwa uchumi wa taifa mbapo sekta ya utalii ndio
muhimili mkuu wa uchumi kwasasa.
Nae Mkurugenzi Jumuiya ya uwekezaji utalii Zanzíbar (ZATI) Julia Bishop
alisema kuwa wanaishukuru sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzíbar kwa
kuwapa mashirikiano kikamilifu jambo linalopelekea sekta ya utalii
kuimarika bila ya pingamizi.
Julia
alisema kwa upande wao wanafanya kazi kubwa kuitangaza Zanzíbar kupitia
sekta ya utalii ambapo pia hufaidika pale wageni wanapoingia nchini .
Nae
mkuu wa msafara kutoka Ubalozi wa Misri Mwandishi Marwa Taufik
alimuelezea Waziri Mbaruok kuridhishwa kwao na mapokezi sambamba na
kujua jinsi gani Serikali ya Mapinduzi ilivyojipanga vyema katika
kuendeleza sekta ya Utalii nchini.
Tawfik
alimuahidi Waziri huyo kuitangaza Zanzíbar kiutalii katika nchi yao ya
Misri kutokana na mazingira mazuri ya kiutalii ambayo Zanzíbar
imejaaliwa kulinganisha na nchi nyingine.
No comments:
Post a Comment