Limezoeleka zaidi kama Bwawa la Viboko la Mikumu lakini ndani ya bwawa hili kuna zaidi ya viboko. Mamba nao wanapatikana kama jinsi ambavyo 'bango' linavyoonyesha na picha zinazofuata. Hapa wageni wanaruhusiwa kushuka kwenye magari yao na kujinyoosha. pia ni sehemu ya kupatia maakuli japo hakuna meza. Kwa ajili ya kupata maakuli wageni watalazimika kula chakula chao kwenye magari. |
Bango liliopo pembeni ya Bwawa hili likitoa maelekezo ya muhimu kwa
wageni na mambo ya kuzingatia wanapokuwepo hapo. Usafi ni moja ya mambo
ya msingi ambayo mgeni anapaswa kuyazingatia anapokuwepo hapa na sehemu
nyingineza ndani ya hifadhi.
Hawa jamaa ndio wanyama wa porini ambao wanaoongoza kwa kuuwa watu
wengi barani Africa (Sub Sahara Africa). Kikubwa ni ukali wao ktk
kulinda himaya zao ambazo zipo kwenye mito. Wengi wanaokumbwa na mikasa
ya hawa majamaa ni wavuvi au watu wanaoenda kwenye mito na mabwawa kwa
shughuli za kuchota maji au kufua
Porini wamepewa jina la Mkasi.
Huyu alikuwa nje ya bwawa akiota jua ili apandishe joto la mwili asiwe
goigoi. Hawa ni wanyama wenye damu baridi, hutegemea joto linalopatikana
kwenye mazingira ili walitumie kupandisha hali ya joto la miili yao.
Wasipofanya hivyo huwa magoigoi hali ambayo huwaweka ktk wakati mgumu wa
kujitafutia chakula.
Unaweza kupata uwiano wa ukubwa wake wa mwili sambamba na mazingira
aliyopo. Bwawa linaonekana dogo lakini mamba wanaoishi humo ni wakubwa
vya kutosha.
No comments:
Post a Comment