Narudia tena, endapo utapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya taifa ya
Serengeti, wasiliana na muandaaji wa safari yako ili kuangalia uwezekano
wa kufanya Hot Air balloon safari ndani ya Serengeti. Japo sasa hivi
huduma za haya mapulizo zipo Tarangire pia. Hutajutia wala kusikitika
kwani ina mvuto wa kipekee na kukupa muonekano wa Uwanda wa Serengeti
kwa namna ambayo hutaitegemea. Hizi ni picha zikionyesha moja ya sehemu
ya safari ya Balloon ndani ya Serengeti, hapa likivuka bwawa la Viboko
lililopo ktk mto Seronera, maeneo ya Seronera ndani ya Hifadhi ya taifa
ya Serengeti.
Ni bwawa lenye idadi ya viboko wa kutosha
Baadhi ya viboko walianza kuhamaki pale balloon liliposogelea bwawa lao.
Njia na mapito unayoyaona nje ya bwawa ni mapito ya wanyama wanaokuja
kunywa maji au njia za viboko wanapotoka na kurudi bwawani. Picha toka
maktaba ya Tembea Tanzania Blog
No comments:
Post a Comment