Gari ndogo yenye nambari za usajili Z 897 DF ikionekana kuvurugika kabisa baada ya kifusi cha dari ya jengo la Makumbusho ya Taifa la Beit al ajaib kuidondokea kufuatia mvua za vuli zinazoendelea kunyesha Zanzibar.
Sehemu ya jengo la Makumbusho ya Taifa la Beit Al Ajaib ikionekana kunyofuka kutokana na mvua za vuli zinazoendelea kunyesha Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia sehemu ya jingo la beit al ajaib ambayo imebomoka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijaribu kuchungulia baadhi ya sehemu ya Jengo la Makumbusho ya Taifa ambalo nyuma ya jengo hilo limepata maafa ya kubomoka.
Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk
Wakati neema ya mvua za vuli ikiendelea kunawiri katika maeneo mbali mbali nchini ikileta faraja zaidi kwa wakulima na wafugaji kwa kupata malisho ya Mifugo yao lakini kwa upande mwengine mvua hiyo hiyo imeonekana kuleta hasara.
Hasara hiyo inaonekana kuikumba Wizara ya Habari,Utamaduni, Utalii na Michezo kufuatia Jengo lake Maarufu la Makumbusho ya Taifa la Beit Al- Ajaib liliopo Forodhani Mjini Zanzibar kubomoka upande wa nyuma wa Jengo hilo.
Kifusi kilichodondoka kutoka kwenye Dari ya Jengo hilo robo yake kimeishiakwenye gari moja ndogo yenye nambari za usajili Z 897 DF inayomilikiwa na Bwana Said Saleh Saidi Mkaazi wa Forodhani ambae alikuwa ameiegesha pembezoni mwa Jengo hilo.
Na Othman Khamis Ame OMPR
No comments:
Post a Comment