Ni miaka takribani 22 imepita tokea nipite kwenye huu uwanja kama
msafiri. Hivi majuzi nilipata fursa ya kupita hapo nikitokea Arusha
kurudi Dar. Muda niliokaa hapo uwanjani ulivuta na kurudisha kumbukumbu
nyingi sana binafsi za enzi hizo. Picha hizi ni baadhi ya picha
nilizoweza kupiga nikiwa hapo. katika kipindi kirefu kwa hivi karibuni,
safari zangu za Arusha zilikuwa ni kwa njia ya Barabara. Uwanja huu wa
ndege ni kiungo muhimu sana kwa sekta ya Utalii hususan kwa vivutio
vilivyopo ktk Ukanda wa utalii wa Kaskazini. japo miaka mingi imepita,
bado muonekano wa uwanja umebaki vile vile hali ambayo ilichangia sana
mimi kuweza kuvuta taswira niliyoihifadhi ya uwanja huu ulivyokuwa enzi
hizo.
Kushoto ni sehemu kwa ajili ya wageni wanaowasili na upande wa kulia ni sehemu kwa ajili ya wageni wanaoondoka.
Mchuma wa Precision Air (ATR 72) ukiwa umeweka pozi kusubiri kupakia
Abiria. Safari za Ndege hizi kutokea Arusha kuja Dar hupitia ZNZ. Hii
ruti ni muhimu kwa sekta ya utalii kwani kwa wageni wengi wanaotoka nje
huanza kwanza kwa kufanya safari za maporini na sehemu nyinginezo na
mwisho huelekea ZNZ kwa mapumziko kwenye pwani kabla ya kukwea mapipa
kurudi makwao. Huu ndio umekuwa mpango wa safari kwa wageni wanaokuja
Tanzania hususan wale ambao hununua package za beach holiday. Siku hii
karibu robo tatu ya abiria wa ndege hii walikuwa ni wageni toka Denmark
ambao walikuwa wametokea Ngorongoro na wote walishuka Zanzibar kuendelea
na mapumziko.
Moja
ya mambo ambayo Mhe Nyalandu alipewa kama lalamiko na wadau wa utalii
ktk Karibu fair ni mpango wa ruti ambao ATCL inautumia. Abiria wanaotoka
Arusha kuja Dar Hupitishwa kwanza Mwanza na kisha wanaletwa Dar. Baadhi
ya wadau walitoa lalamiko hilo ambao na wao walilipata toka kwa wageni
wao.
No comments:
Post a Comment