Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akitoa salamu zake kwenye hafla ya
Usiku wa Tarangire iliyokuwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani na
pia kumuaga aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire Ndg. Martin
Laiboki ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uhifadhi na Ekolojia
TANAPA Makao Makuu, hafla hiyo ilifanyika katika Hifadhi ya Tarangire.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo (wa pili kulia) akimkabidhi Kamba
Ndg. Martin Laiboki kama ishara ya zawadi ya Ng’ombe aliyozawadiwa na
Uongozi na Wafanyakazi wa Hifadhi ya Tarangire kwenye hafla ya jioni ya
kumuaga baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uhifadhi na Ekolojia
TANAPA Makao Makuu, awali Ndg. Laiboki alikuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi
ya Tarangire.
Mwanamuziki
wa Bendi ya FM Academia Nyoshi El – Saadat (katikati) akifungua
Champaign kwenye hafla ya Usiku wa Tarangire iliyofanyika hifadhini hapo
ambapo Bendi hiyo FM Academia ilitumbuiza na pia iliimba kibao maalumu
kinachohamasisha utalii wa ndani kwa watanzania.
Mkuu
wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba/miwani), Mkuu wa Mkoa
Manyara Elaston Mbwilo (kulia kwa Dr. Nchimbi) Uongozi na wafanyakazi
wa Hifadhi ya Taifa Tarangire wakiserebuka kwa muziki wa Bendi ya FM
Academia wakati wa hafla ya Usiku wa Tarangire iliyofanyika hifadhini
hapo.
Wanamuziki
wa Bendi ya FM Academia wakionesha vitu vyao wakati wa Hafla ya usiku
wa Tarangire iliyofanyika kwenye hifadhi hiyo ya Taifa.
No comments:
Post a Comment