Ni Katika kile kinyang'anyiro cha kupata vivutio asilia saba vyenye
maajabu toka barani Afrika. Kinyang'anyiro ambacho kilirindima mwaka
jana kwa wadau kupigia kura vivutio 11 vilivyokuwa vikishindanishwa.
Mlima Kilimanjaro, Wanyama wanaohama wa Serengeti na Ngorongoro crater
ndio yalikuwa maajabu toka Tanzania ambayo yalikuwa yameteuliwa kupigiwa
kura. kwa kifupi, vivutio vyote vitatu toka Tanzania vimeweza kufanya
vyema.
Taarifa ya vivutio vitatu kutoka Tanzania kuingia kwenye orodha ya
vivutio 7 vya ajabu barani Afrika imewekwa wazi hii leo jioni huko mjini
Arusha ambako kulikuwa na sherehe rasmi ya kuvitaja vivutio
vilivyoingia kwenye orodha hii baada ya zoezi la kupiga kura kusitishwa
mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana. Katika hafla hiyo, Waziri mkuu wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio alikuwa mgeni rasmi. Matokeo hayo
yalitangazwa na Dk, Phillip Imler ambaye ni rais wa taasisi ya Seven
Natural wonders of the world.
Vivutio vingine viliweza kuingia kwenye orodha hii ni Okavango Delta,
Red Sea Reef, Jangwa la Sahara na Mto Nile. Tanzania ndio nchi pekee
iliyoweza kuingiza vivutio 3 kwenye orodha hii kwa mwaka huu. Ngwesa Tourism
blog inatoa pongezi kwa wote waliotikia wito na kupiga kura na
kuiwezesha nchi yetu kutoka kifua mbele kwa kuingiza vivutio 3 kwenye
orodha hii. Tunaweza pale kila mmoja akishiriki kikamilifu.
No comments:
Post a Comment