Walking Safari ktk hifadhi na mapori ya akiba ni namna moja ambayo
binafsi nakuwa naipa nafasi sana ktk mipangilio ya safari zangu za
porini. Inabaki kuwa njia moja inayoniweka karibu kabisa na wanyama pori
na mazingira yao katika hali ambayo ni asili na ya kipekee. Kwa hapa
Tanzania, karibu hifadhi zote za taifa zinatoa fursa hii baada ya mgeni
kulipia gharama husika. Mgeni husindikizwa na Ranger mwenye silaha
kipindi chote cha safari, na Ranger hupanga safari kulingana na matakwa
na mategemeo ya mgeni wake. Jambo la muhimu kwa mgeni ni kujiandaa na
pia kufuata maelekezo ya ranger wake kipindi chote wanapokuwa porini.
Jambo jingine ni kuhakikisha mnatembea kama kundi moja kipindi chote
(kama mpo wengi).
Hili ni kundi la mabachelor (wote wana mapembe) wakitupisha njia na kuendelea kula.
Na wanyama (wenyeji wetu) walipigwa na butwaa kutuona tukiwa tunatembea
kwa miguu wakati wao wamezoea kuwaona wageni wao wakiwa ndani ya magari
Nothing stands between you, the wildlife and the wilderness in gerenal...
Hizi sio njia za kwenda sokoni, ni mapito ya wanyama wanapokuwa wakienda
kunywa maji. Kulikuwa na bwawa la maji eneo karibu na makutano haya.
Nilipata wasiwasi kwani ninavyojua mimi kwenye njia kama hizi ndipo
ambako Sharubu hutega mitego yake. Tulipita salama na kumaliza misele
yetu salama bila ya kukutuana na sharubu, nyati au masikio kwa karibu.
Kwa karibu zaidi.
Ulinzi kamili
Game walk unaweza kumaliza kwa namna mbili, moja ni kurudi
pale ulipoanzia au kusonga mbele na gari yako ikakufuata ndani ya
hifadhi mahali na muda ambao mnakubaliana na dereva. Picha zote ni toka ktk maktaba
ya TembeaTz
No comments:
Post a Comment