Mkurugenzi
wa Idara ya Utalii , Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Bw. Ibrahim
Mussa (kushoto) akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii ya
China Bw. Zhu Shanzhong juu ya masuala mbalimbali ya uhusiano baina ya
nchi hizi mbili hususan katika sekta ya utalii wa Tanzania katika soko
la China.
Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kushoto) na Kaimu Mhifadhi wa Mamlaka ya
Ngorongoro Bruno Kawasange wakifuatilia mazungumzo hayo.
Balozi
wa Tanzania nchini China Philip Marmo (kulia) na Mbunge wa Ngorongoro
Mhe. Kaika Telele wakifuatilia mazungumzo baina ya serikali ya Tanzania
na China kuhusiana na sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki (kulia) na Mkurugenzi
Msaidizi wa Malikale John Kimaro wakifuatilia mazungumzo hayo kwa
umakini.
Viongozi wa Serikali ya China wakifuatilia majadiliano. (Picha zote na mdau Pascal Shelutete, TANAPA)
Mkurugenzi
wa Idara ya Utalii Ibrahimu Mussa (kushoto) akipokea zawadi maalum ya
stempu mbalimbali za China kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya
Utalii nchini China Zhu Shanzhong mara baada ya kumalizika kwa
mazungumzo yao.
Mkurugenzi
wa Utalii Ibrahimu Mussa na Balozi Philip Marmo wakiwa na Makamu
Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii ya China Bw. Zhu Shanzhong
…………………………………………….
Pascal Shelutete, Beijing
Matangazo ya moja kwa moja ya
Mzunguko wa Nyumbu wahamao katika Hifadhi ya Serengeti katika
Televisheni ya Taifa ya China yameongeza mwamko wa wachina kutembelea
Tanzania kama watalii. Haya yalisemwa jana na Makamu Mkurugenzi wa
Kurugenzi ya Utalii ya China Zhu Shanzhong alipokutana na ujumbe kutoka
Tanzania jijini Beijing China.
Shanzhong alisema kuwa Hifadhi ya
Serengeti ambapo vipindi kadhaa vimesharushwa tangu mwezi januari mwaka
huu nchini China, inaendelea kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa
wananchi wa China na kuelezea matarajio yake kuwa matangazo haya
yataweza kuongeza idadi ya watalii nchini katika muda mfupi ujao.
Alisema kuwa ziaraya hivi karibuni
iliyofanywa na Rais wa Ji Xinping nchini imeendelea kuitangaza Tanzania
nchini China na kuongeza kuwa upekee wa vivutio vya utalii ni mtaji
mzuri unaopaswa kutumika vizuri kutangaza utalii na hivyo kuongeza pato
la taifa.
Mapema Makamu Mwenyekiti huyo
alieleza haja ya kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya sekta za
utalii kwa nchi hizi mbili na kutaka kuandaliwa kwa rasimu ya Hati ya
Makubaliano itakayobainisha maeneo muhimu ya kushirikiana kwa kuwa na
mipango thabiti ya muda mrefu na mfupi.
Katika mkutano huo, Shanzhong
aliomba ridhaa ya Tanzania kuridhia ombi la China la kuanza kutumia kwa
lugha ya kichina kuwa mojawapo ya lugha rasmi zitakazotumika katika
vikao vya Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii. Alieleza kuwa nchi yake
imepeleka ombi hilo makao makuu ya shirika hilo ambayo yanahitaji
kuungwa mkono na zaidi ya nusu ya nchi wanachama wa shirika hilo.Ujumbe
wa Tanzania unaoongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Ibrahim Mussa
uliahidi kuwa Tanzania itaunga mkono ombi hilo kabla ya kufanyika kwa
mkutano mkuu wa UNTWO mapema mwezi Agosti mwaka huu nchini Zimbabwe na
Zambia
No comments:
Post a Comment