Rais
Barack Obama wa Marekani anatarajiwa kuzuru bara la Afrika mwezi ujao
ambako atatembelea mataifa ya Senegal, Afrika kusini na Tanzania.
Kwa
mujibu wa taarifa ya msemaji wa Ikulu ya Rais nchini Marekani Jay
Carney, rais Obama amepangiwa kufanya ziara hiyo kati ya tarehe 28 mwezi
ujao hadi tarehe 3 mwezi Julai ambako atakutana na viongozi wa
serikali, biashara na wa mashirika ya kijamii kwa lengo la kuhimiza
amani na ustawi wa bara Afrika.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa Rais huyo wa Marekani atasisitiza umuhimu wa
uhusiano kati ya Marekani na nchi za Afrika ikiwemo kupanua ukuaji wa
kiuchumi, uwekezaji na biashara pamoja na kuboresha asasi za
kidemokrasia.
Mara ya mwisho kwa rais Obama kutembelea nchi ya bara Afrika ni mwaka 2009 alipozuru Ghana.
No comments:
Post a Comment