mwananchi wa huko waarabuni akichukua picha ya kakakuaona kwenye simu yake
Mnyama Kakakuona akiwa amewekewa viu mbalimbali ili achague kimoja ambacho hutoa ishara ya kutokea kwa kitu hicho hapo mbeleni
Mnyama inayesemekana wa ajabu Kakakuona na ambaye huonekana kwa nadra
sana ameonekana jana katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. Mnyama huyo
anapoonekana wanaomuelewa wanamuwekea vitu mbalimbali ikiwa kama kumtaka
atabiri ni nini kitatokea kwa kipindi kijacho. kama akielekea kwenye
maji wengi huwa wanadai ni mvua za kutosha. Jana katika vitu
alivyowekewa mnyama huyo alielekea kwenye mtungi wa gesi na
kuulambalamba ambapo kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo hayo ya imani
wanadai kutakuwa na gesi ya kutosha maeneo hayo na hasa ukizingatia
tayari maeneo hayo yashagunduliwa gesi na inasubiriwa tu kazi ya
uchimbaji iendelee.
Sina uhakika sana kama haya mambo ni kweli au ni mambo tu ya Imani
mbofumbofu!1 kam ani kweli basi nadhani kila nyumba bongo itaatumia gesi
na kusahau mkaa; magari yote bongo tutatumia gesi na kuachana na Kiwese
ambacho kinapanda bei kila kukicha.
Kakakuona akiwa katika pozi
Kakakuona akiusogelea mtungi wa gesi
No comments:
Post a Comment