nmb

nmb

Tuesday, April 23, 2013

FAHAMU JINSI YA KUTUMIA MAJI KAMA TIBA - 2

Hii ni sehemu ya pili na ya mwisho kuhusu unywaji wa maji kama tiba mbadala ya maradhi mbalimbali.  Tafadhali endelea kusoma ili  kujua namna ya kutumia maji kama tiba.

PILI: Kutokana na shinikizo hilo la maji la ghafla, masalia na vipande vya vyakula ambavyo huganda kwenye kuta za utumbo mdogo, husombwa na maji hayo pamoja na gesi na vitu vingine ambavyo havikusagwa na kutupwa kwenye utumbo mpana tayari kutolewa kama uchafu. Hali hii huuacha utumbo mdogo ukiwa safi na kuzipa seli uhai mpya!

TATU: Utumbo siyo sehemu pekee inayonufaika na tiba hii ya maji, bali chembechembe hai (cells) zote za mwili huwa zimepewa uhai na nguvu mpya. Maji yanaponywewa baada ya mwili kutoingiza kitu chochote kwa kipindi cha saa 8 – 10, mwili huyapokea maji hayo kwa ‘kiu’ kubwa na kuyasambaza katika seli zote za mwili.
Vijidudu nyemelezi (free radicals) na vitu vyote vyenye sumu ambavyo huganda kwenye seli, kimsingi hushinikizwa kujiondoa vyenyewe kutoka kwenye seli hizo, hivyo kuurahisishia mfumo wa kusafisha mwili kuondoa mwilini sumu na vitu visivyotakiwa kwa urahisi.

TAHADHARI:
Kwa mgonjwa anayetumia tiba hii ya maji, kuna mabadiliko au usumbufu fulani anaoweza kuupata katika siku 3 au 7 za mwanzo. Anaweza kuumwa na kichwa au mwili na kuhisi kama kichwa chake ‘kinaogelea’. Vile vile anaweza kutokwa sana jasho, kusikia kichefuchefu au kama si hivyo, anaweza asijisikie vizuri tu.
Hayo yasikutie hofu, hayo SIYO MADHARA (side effects), bali hiyo ni dalili kwamba mwili umeanza kuondoa sumu zilizoganda kwenye seli zake. Kwa kuwa tiba ya maji haina madhara yoyote, unapoona dalili hiyo usiache, endelea kama kawaida, kama utashindwa basi punguza kidogo kiasi cha maji unachokunywa.
Baada ya siku kadhaa kupita, mgonjwa hurejea katika hali yake ya kawaida na hiyo huwa ni dalili kwamba mwili umeanza kutakasika. Hali ikirejea kama kawaida, mgonjwa hana budi kuendelea na kiasi kilekile cha maji kilichopendekezwa.

ZINGATIA
Ingawa tiba ya maji ni nzuri kwa wagonjwa wengi wa figo na moyo, lakini wenye matatizo MAKUBWA ya magonjwa hayo, wanashauriwa kujaribu tiba hii baada tu ya kupata mwongozo sahihi na ruhusa ya daktari anayeijua vizuri hali ya mgonjwa wake.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis