Haya ndio mabanda wanamolala wageni wanaopanda mlima Kilimanjaro kwa
njia ya Marangu. ifahamike ya kwamba, ni njia ya Marangu pekee (kwa
mlima Kilimanjaro) ambapo mgeni anakuwa na fursa ya kulala kwenye banda.
(Huts). Wapandaji wa njia nyingine wanalala kwenye mahema madogo au
makubwa. Picha juu ni moja ya mabanda yaliyopo kwenye kituo cha Mandara.
Banda hili limegawanywa sehemu mbili ambako kila sehemu ina uweze wa
kulaza wageni wanne. Mabanda yana solar hivyo wageni wanakuwa na uhakika
wa mwanga japo ukitaka kuchaji simu au kamera inabidi uende kwenye
banda la wasimamizi ambako wao ndio wana socket. Vyumbani kuna switch ya
taa na taa yenyewe tu. Kwa anayepanda kwa njia ya Marangu, atalala
kwenye huts kama hizi katika kituo cha Mandara na Horombo. Kituo cha
Kibo kina chumba kilichojengwa kwa mfumo wa bweni lenye vyumba kadhaa
ndani yake. Lipo tofauti kidogo na hizi huts za Mandara na Horombo.
Hali ilivyo ndani, hii ni sehemu ya upande mmoja wapo wa banda
tulilolala sisi. upande wa pili kuna sehemu nyingine yenye uwezo wa
kulaza wageni wanne. mpango ulivyo ndani ni wageni watatu wanalala
kwenye hivi vitanda vya chini wakati mmoja analala hapo juu. Magodoro
unayakuta ktk hut isipokuwa mgeni unalala kwenye sleeping bag yako
uliyokuja nayo.
No comments:
Post a Comment