Nani kasema ndizi ni kwa Bukoba, Kilimanjaro na Mbeya pekee? hapa ni Madizini Morogoro wanasema nao Moro wanalima ndizi
Kwa wenyeji wa Morogoro kawaida ndizi huliwa zikiwa mbivu au kama vitafunwa (kwa kunywea na chai). Huwezi ukapikiwa ndizi halafua ukasema kuwa leo nimekula chakula. Hata kama watachanganya na nyama bado ni vitafunwa tu. Chakula cha heshima kwetu ni wali! Angalia hii mikungu ya ndizi
Ndizi tamu kutoka Morogoro. Msichana mrembo akiziweka sawa
Mfanyabiashara
wa ndizi katika kijiji cha Magole wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro,
Fadhil Seleman akikokota baiskeli iliyosheheni mikungu ya ndizi baada ya
kununua shambani kisha kuuza kwa wenye m,angeni kijijini hapo kwa bei
ya jumla ya sh 2,000 hadi sh 2,500.
No comments:
Post a Comment