TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UHAMASISHAJI WA KUPIGIA KURA MLIMA KILIMANJARO,
BONDE LA NGORONGORO NA TUKIO LA KUHAMA WANYAMA
KATIKA HIFADHI YA SERENGETI KATIKA SHINDANO LA
MAAJABU SABA YA ASILI KATIKA BARA LA AFRIKA
Photo: Honorable Ambassador Khamis S. Kagasheki,
Tanzania’s Minister of Natural Resources and Tourism and Luke Bailes,
CEO and Founder of Singita.
Hivi karibuni pamekuwa na shindano jipya
lijulikanalo kama seven Natural Wonders linaloshindanisha vivutio
mbalimbali vya asili vinavyopatikana katika kila bara. Shindano hilo
linaloendeshwa kwa kupiga kura kupitia tovuti ya http://sevennaturalwonders.org
linashindanisha vivutio vya utalii kumi na viwili (12) katika bara la
Afrika. Tanzania ni nchi pekee yenye vivutio vingi katika orodha hiyo.
Vivutio vya Tanzania ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na
hifadhi ya Serengeti. Watanzania na watu wote duniani wanahamasishwa
kuvipigiakura vivutio hivyo vitatu
Ili kurahisisha upigaji kura kwa vivutio vya Tanzania, Bodi ya Utalii Tanzania imewaomba waandaji wa shindano hilo kuandaa tovuti maalum ambayo ni http://sevennaturalwonders.org/tanzania/ itakayomuhitaji mpigakura kutuma barua pepe yenye kichwa cha habari “TANZANIA” inayoorodhesha vivutio hivyo vitatu (3), na vivutio vingine visivyozidi vinne (4) vilivyopo Tanzania ambavyo mpigakura anaona vinafaa viwemo katika orodha ya maajabu saba ya asili ya Tanzania, kwenda kwenye anuani hii vote@sevennaturalwonders.org. Kwa maelezo zaidi kuhusu vivutio vya utalii Tanzania tembelea www.tanzaniatourism.go.tz.

Shindano hili linaweza kuwa fursa nzuri kwa
Tanzania kujitambulisha pamoja na kuitangazia dunia kuwa Mlima
Kilimanjaro, ambao ni mlima mrefu kuliko yote barani Afrika; Hifadhi ya
Serengeti, ambapo tukio la kuhama wanyama hutokea kila mwaka; na eneo la
Ngorongoro, ambalo ni urithi wa dunia wa asili na utamaduni (natural
and cultural World Heritage Site), vyote ni vivutio vilivyopo hapa kwetu
Tanzania.
Vivutio vitakavyoshinda vitatangazwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani na kupewa hadhi zaidi ya kimataifa.
Tumia fursa hii kupigia kura vivutio vyote vya Tanzania ili viweze kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili ya bara la Afrika.

Imetolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji
BODI YA UTALII TANZANIA
BODI YA UTALII TANZANIA
No comments:
Post a Comment