SANII wa muziki wa kizazi kipya,Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewataka watanzania kulipigia kura bonde la Ngorongoro kuwa moja ya maajabu saba ya Afrika na pia kujenga tabia ya kutembelea vivutio vya utalii vya ndani.
Akizungumza
mjini Ngorongoro, Diamond ambaye alikuwa huko kujionea bonde hilo
ambalo ni la kipekee ulimwenguni, amesema hakuwahi kufikiria kwamba kuna
sehemu nzuri ambayo hata watanzania wanaweza kwenda kutembea na
kujionea vivutio vilivyopo.
“Hii
ni mara yangu ya kwanza kufika hapa, lakini kwa kweli nimeshangazwa na
jinsi palivyo pazuri, wanyama, mito ambayo inapita huku chini, mi huwa
naona kwenye televisheni tu katika kile kipindi cha National Geography
cha DSTV lakini sikujua kama mambo haya yapo kweli kwetu.
“Nawaomba
watanzania wenzangu waweze kutembelea Ngorongoro na vivutio vyetu vya
utalii kwa sababu kuna mengi ya kujifunza, leo kama isingekuwa Afrika
sidhani kama kungekuwa na kipindi kama National Geography, na gharama za
kuja huku si kubwa, hatupaswi kuogopa, hivi ni vitu ambavyo
vinawezekana kabisa suala ni kujipanga,” amesema.
Amesema
wenzetu kutoka Ulaya wamekuwa wakijipanga kuweza kutembelea sehemu
Fulani jam bo ambalo linawafanya waweze kutembelea nchi nyingi kufanya
utalii.
“Pamoja
na kuja kupunguza mawazo lakini sehemu kama hii inasaidia kuelemisha,
mwito wangu kwa watanzania wenzangu, mashule hata vyuo waweze kuja hapa,
inakuwa rahisi zaidi kumfundisha mtoto kuhusu Simba, Twiga, au bonde la
Ngorongoro kwa kumuonyesha hiki kiko hivi, nadhani kama watoto watakuwa
wanasoma kwa vitendo hawawezi kushindwa mitihani yao kwa sababu
kumbukumbu inabaki kichwani kwa kile walichokiona,” amesema.
Msanii
huyo alikwenda Ngorongoro baada ya kumalizika kwa tamasha la Fiesta
ambapo alikuwa mmoja wasanii waliofanya vizuri. Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro ilimualika Diamond huko. Ngorongoro ni moja kati ya vivutio
vya Tanzania vinavyotakiwa kupigiwa kuingia katika maajabu saba ya
Afrika
No comments:
Post a Comment