mto ulivyokuwa zamani
JUHUDI za Serikali na wadau wa uhifadhi na mazingira duniani kote za kuuokoa mto Ruaha Mkuu usikauke ni dhahiri sasa zinaanza kugonga mwamba baada ya mto huo kuendelea na kasi yake ya kujigeuza kutoka mto wa mwaka mzima kuwa wa msimu.
Kufuatia hali hiyo maisha
ya watu na wanyama na viumbe wengine hai katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha na
kwingineko unakopita mto huo yako hatarini ikiwa mto huo utakauka kabisa.
Takribani miaka saba
iliyopita mamia ya wafugaji na maelfu ya mifugo iliyokuwa ndani ya eneo oevu la
Ihefu waliondolewa na serikali kwa lengo kulinda eneo oevu la Ihefu ambalo
ndiyo chanzo kikuu cha mto Ruaha Mkuu lisiharibiwe na wafungaji hao na hivyo
kuendelea kupeleka maji katika mto huo.
Ilitarajiwa kwamba baada
ya bonde la Ihefu kurejea katika uasili wake,mto Ruaha Mkuu ungetiririsha maji
mwaka mzima lakini kuanzia eneo la Lunda,ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha,mto
huo umekauka kabisa na hivyo kuzua hofu kubwa.
Mhifadhi Mkuu wa hifadhi
ya Ruaha – RUNAPA Stephano Qolli anasema athari za kukauka kwa mto Ruaha Mkuu
sasa wameanza kuziona dhahiri na kulaumu kilimo cha umwagiliaji mashamba
makubwa upande wa juu wa mto huo maeneo ya wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya.
Mto Ruaha Mkuu unategemewa
sana katika uchumi wa Taifa kupitia kilimo, uhifadhi na uzalishaji nishati ya
umeme katika bwawa la Mtera na Kitadu na kama isingekuwa juhudi za Wizara ya
Nishati na Madini,Taifa hivi sasa lingekuwa katika mgawo mkubwa wa umeme
kutokana na hali ya bwawa la Mtera kuwa mbaya zaidi ikilinganishwa na miaka
minne iliyopita.
1 comment:
Please visit our website ruahanationalpark.weebly.com ..Ruaha is 'Tanzania's Best Kept Secret' and the largest park in East Africa. The site has everything you need to know about Ruaha!
Post a Comment