this photo from tanzaniaparks.com |
Ni moja ya hifadhi za taifa ambazo ni kama hazimu lakini zipo. Ipo
mkoani Kilimanjaro, katika wilaya ya Same. Ni moja ya hifadhi za hapa
nchini ambako Mbwa mwitu pamoja na vifaru wanatunzwa kwa lengo la
kuzaliana ili kuweza kurudisha idadi yao ktk mapori na hifadhi nyingine
hapa nchini. Awali ilikuwa ni pori la akiba mpaka miaka ya hivi karibuni
ilipopandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya taifa. Ni Hifadhi yenye
mkusanyiko wa wanyama wengi utakaowategemea kuwakuta kwenye hifadhi
nyinginezo. Kitu kimoja cha kipekee kwa Mkomazi ni kwamba hutumika kama
kituo kwa ndege ambao huhama kati ya bara Ulaya na Afrika. Ni hifadhi
ambayo huwavutia sana wageni wanaopenda kuangalia aina mbali mbali za
ndege. Ndege wanaohama hutumia maeneo ya hifadhi kama vituo vyao vya
kupumzikia wakiwa wanaelekea kusini mwa Afrika au kipindi wanapokuwa
wanarudi makwao - Bara la Ulaya.
Picha juu ni moja ya njia zinaweza kukufikisha kwenye Hifadhi ya Taifa
ya Mkomazi. Hii njia ipo katika barabara kuu ya Arusha-Dar. Njia
nyingine inayoweza kukufikisha Mkomazi ni ile inayoingilia pale Same
"mjini". Hii ipo karibu na geti kwani inaelezwa ya kwamba ni mwendo
usiozidi Kilometa 10 tokea h Same, unakuwa tayari ndani ya eneo la
hifadhi. Hiyo ya kwenye picha juu ni umbali wa kilomenta 66 kama
zinavyoonekana ktk bango. Njia hii imezoeleka na wengi kama njia ya
kwenda Gonja. Kwa anayetumia njia hii ataingilia geti lijulikanalo kama
Njiro. Kwa yule atakayeingilia njia ya Same ataingia ktk hifadhi kupitia
geti la Zange.
Njia kuu ya DSM - Arusha ikionekana huku njia panda ya kuelekea Gonja
hadi hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ikionekana. Milima inayoonekana kwa
nyuma ni safu ya Milima ya Usambara.
No comments:
Post a Comment