Kuvuka mto Mara ni ishara ya kuonyesha kuwa Migration imeshaingia Nchini na kuwa ipo ktk Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Hulazimika kuogelea ili kuweza kuvuka salama. Wengi husombwa na maji na
kufa na wengine huishia kwenye midomo ya Mamba ambao husubiri tukio
hili kwa hamu kubwa. wanapovuka mto Mara huwa wanatoa fursa ya mamba wa
mto Mara kuweza kupata mlo wa uhakika ambao utawalinda kwa kipindi
kirefu mpaka nyumbu hawa watakaporudi tena kuelekea Kaskazini.
Wanahabari na wageni kadhaa ni baadhi ya wageni waliolishuhudia tukio
hili hivi Karibuni ktk hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kundi la Nyumbu
ambalo limeshavuka mto na kuingia Tanzania linaonekana nyuma yao.
(Shukran ya picha kwa Mdau Bonny toka Arusha)
Kila
mwaka, nyumbu pamoja na wanyama wengine kama pundamilia na swala
hufanya mzunguko maalum unaochukua miezi 12 ya mwaka ambapo miezi kumi
kati ya hiyo huwepo nchini katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na
iliyobaki hutumiwa na wanyama hao katika eneo la Hifadhi ya Masai Mara
nchini Kenya.
Mwaka
huu msafara huu unaohusisha wanyama zaidi ya Milioni Moja na Nusu na
ambao hutembea katika mzunguko wa takribani Kilometa 1,000 umewahi sana
kurejea nchini ukitokea mapumziko na hii kwa mujibu wa taarifa za
kitaalamu inatokana na kuwahi kunyesha kwa mvua katika eneo la Serengeti
ambapo imesababisha kuwepo na nyasi nzuri ambazo ni chakula muhimu kwa
wanayama hawa.
Changamoto
kubwa wanayokutana nayo msafara huu mara unaporejea nyumbani ni tukio
la kuvuka Mto Mara ambao umejaa wanyama wakali aina ya mamba na viboko
ambao nao huwa ni msimu wao wa kujipatia chakula kwa kuvizia na hatimaye
kuwakamata wanyama hawa mara wanapovuka mto.
Watalii
kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakifurika katika Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kushuhudia tukio hili adimu la kuvuka Mto Mara ambalo
wengi wao wamekuwa wakiliona kupitia filamu mbalimbali zilizotengenezwa
katika eneo hili.
Asante
Pascal Shelutete,TANAPA
kwa habari pamoja na picha
No comments:
Post a Comment