Haikuweza kufahamika mara moja mnyama aliyeuwawa na kuning'inizwa mtini
kwa namna hii lakini ni dhahiri mnyama anayehusika kwa uhifadhi wa
akiba Kwa style hii ni Chui aka wa juu. Katika familia ya paka
wawindaji, chui huhifadhi mawindo yake juu ya mti ambako wanyama wenzake
hawawezi kuYAfikia kirahisi na kumpokonya windo lake. Style hii
humwezesha chui kujihakikishia mlo na pia kukwepa adha ya kula chakula
kwa mkupuo na haraka kwa kuwa ana uhakika na friji lake halivamiwi
kirahisi. Ukiangalia vyema utabaini ya kwamba ameenda kuuficha huo mzoga
wake kwenye matawi madogo. kwa hapo alipoweka, hata wale ndege wa
mizogo Tai (tumbusi) hawewezi kuufikia kwani anakuwa anazuiwa na matawi.
Kumbuka ya kwamba Tumbusi ni moja ya ndege wakubwa wanaopatikana kwenye
mapori na hivi huhitaji sehemu ya wazi kuweza kutua na kuruka.
Chui ni mnyama ambae hujenga na kulinda himaya yake.Kwenye himaya ya
chui mmoja (dume) si rahisi kukuta chui mwingine ambaye hana uhusiano na
mwenye kaya (territory). Na wao pekee ndio wenye uwezo mzuri wa kukwea
miti hata ile iliyonyanyuka wima na kuweza kufika kule kwenye fito
nyembamba. Akiweka huku basi ana uhakika wa kukuta windo lake likiwa
salama. kama kuliwa basi litakuwa limeliwa na jamaa au ndugu yake. Chui
mmoja akiingia kwenye kaya ya mwenzie hufukuzwa kama mbwa mwizi na mara
nyingi akibisha hutembezewa kichapo kikali.
(picha toka kwa -KK Wildness Safaris Tanzania)
No comments:
Post a Comment