Na; Faraji Feruz
Mtwara
Wito umetolewa kwa
serikali kuona umuhimu wa kutenga bajeti kwa ajili ya shughuli za
kiutamaduni hapa nchini, ili kusaidia kuendeleza, kuhifadhi,
kuthibitisha na kuhimiza mila na desturi zinazoendelezwa katika baadhi
ya maeneo hapa nchini.
Mkurugenzi mwenza
na mratibu wa makuya na mahusiano ya umma, kutoka taasisi isiyokuwa ya
kiserikali ya ADEA, Phillipo Lulale ametoa wito huo, mbele ya waandishi
wa habari, wakati akitambulisha tamasha la nne la ngoma za asili,
maarufu MAKUYA mwaka 2012.
mesema kuwa ni
muhimu kwa serikali kuwa na bajeti yenye msingi wa kuendeleza tamaduni
za mtanzania, kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia
yanayoendelea kutokea katika bara zima la Afrika na dunia kwa ujumla, na
hivyo kuhatarisha kutoweka kwa urithi huu katika muda mfupi ujao.
Lulale amesema kuwa
dhumuni kubwa la tamasha hilo la MAKUYA, ni kujenga uelewa kwa jamii ya
ndani na ile ya kimataifa juu ya utajiri na urithi wa ngoma za asili,
kukuza utamaduni katika mkoa wa mtwara, kusaidia utunzaji na uendelezaji
wa ngoma za asili na kuukumbusha umma kwa ujumla uwepo wa utamaduni wa
ngoma za asili kusini mwa Tanzania.
Nae mratibu wa
tamasha la MAKUYA, toka taasisi ya ADEA, Dominic Chonde amesema kuwa
tamasha hilo litakalofanyika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
mtwara, kuanzia novemba 17 hadi 18, litahusisha vikundi 15 vya ngoma ya
sili kutoka manispaa na halmashauri zote za mkoa wa mtwara, huku
likijumuisha makabila makuu matatu ya wamakonde, wamakua na wayao.
Amesema kuwa
tamasha la mwaka huu, ambalo ni la nne, tangu kuanzishwa rasmi mwaka
2008, litagharimu kiasi cha shilingi milioni 60, na kufadhiliwa na
uablozi wa Finland, British Gas, Wentworth Afrika Foundation, na Odjell
Drilling, ambapo shughuli mbalimbali zikiwemo ngoma za asili, maonesho
ya wazi ya mafundi wa jadi, mabanda ya kuonesha vifaa vya asili na
michezo mbalimbali ya jadi zitafanyika katika tamasha hilo.
source: the chief
No comments:
Post a Comment