Wilfred Moshi akipeperusha bendera ya Tanzania kileleni Mlima Everest
Safari ya kukwea Mlima Everest ikipamba moto
Wilfred Moshi safarini kuelekea kileleni
Frank Eyembe wa Urban Pulse na Wilfred Moshi baada ya kupanda moja ya milima mirefu Uingereza iliyopo Holyrood Park EdinburghFrank Eyembe wa Urban Pulse na Wilfred Moshi baada ya kupanda moja ya milima mirefu Uingereza iliyopo Holyrood Park Edinburgh
Imeandikwa na Freddy Macha kwa ushirikiano na Urban Pulse
Picha zote hisani ya Wilfred Moshi na Urban Pulse
Kwa
mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi yetu kijana Wilfred
Moshi, Mbongo wa kawaida tu (anayefanya kazi ya upagazi kuwahudumia
watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro), ameweka rekodi mpya ya kuwa
Mtanzania wa kwanza kupanda Everest - mlima mrefu kushinda yote duniani.
Hivi karibuni,
Moshi, alialikwa majuma matano nchini Uingereza kutembelea shule
mbalimbali za Scotland akakutana na takribani wanafunzi 5,000 .
Wanafunzi
walitaka kufahamu namna alivyopanda mlima Everest wenye mita 8,848
(futi 29, 029). Mlima huu mgumu kuukwea kuliko yote ulimwenguni umewahi
kupandwa na na watu 4,000 toka ulipoanza kufikiwa kileleni na Edmund
Hillary na Sherpa Tenzig Norgay mwaka 1953. Kati ya hao 200 walifariki.
Mwaka huu wanne wameshafariki wakiijaribu shughuli hii
inayochukua miezi miwili na kugharimu Dola 100,000 (Shilingi milion
157,500,000) Linganisha na mlima Kilimanjaro unaodai siku tano na gharama (ikiwepo vifaa husika) Dola 2,000 (Shilingi milioni 3, 161).
Wilfred Moshi ni Mtanzania wa kwanza na Mwafrika wa tatu kufikia kilele cha kitendawili hiki Mei 19 2012 (kilichoitwa “Chomolungma” na wenyeji kabla ya kubatizwa jina la Everest na Waingereza enzi za ukoloni).
Wilfred
aliyezaliwa mwaka 1979 na kumaliza kidato cha sita shule ya Kilimanjaro
Boys, amekuwa akipanda mlima Kilimanjaro tangu angali bado shuleni na
miaka 19.
Mara
baada ya kuwasili Edinburgh, Scotland alikaribishwa bungeni akakutana
na Waziri wa Sheria mheshimiwa Kenneth MacAskill na viongozi wengine.
Safari ilikirimiwa na shirika la “Twende Pamoja” lililoanzishwa na Mike
Knox miaka 30 iliyopita. “Twende Pamoja” imejenga ushirikiano kati ya
wanafunzi wa Scotland na shule 34 za Kitanzania. Ni moja ya mashirika,
watu binafsi na wafadhili mbalimbali ulimwenguni waliochangia fedha za
kumwezesha Moshi kupanda mlima Everest.
Balozi
wetu Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe vile vile alisafiri toka
London kumtembelea Wilfred Moshi na kumpa heko. Umbali wa London had
Scotland ni kama Dar es Salaam hadi Kigoma!
Kwanini Moshi anahusudu kupanda milima?
Ukweli
sisi bado hatuoni umaana (au umuhimu) wa kupanda milima. Anasema lengo
lake lilikuwa kutimiza ndoto ya Mtanzania wa kwanza kupanda Everest.
Pili, upandaji milima ni moja ya njia zinazoweza kusaidia kujenga jamii
kwa misaada na fadhila za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO).
Tujiulize vipi alisaidiwa na watu wengi namna hiyo kuchangia fedha
takikana? Tatu, Moshi amethibitisha ukiwa na moyo na jitihada unaweza
kufanya lolote. Ushujaa na ushupavu wake utasaidia kuwahamasisha
Watanzania kuwa ukitaka kufanya jambo lolote lile unaweza ili mradi uwe
na moyo na nidhamu.
Mpanda
milima mashuhuri, Mike Hamill, aliyeshakwea milima yote mikubwa saba
duniani anasema katika kitabu chake kipya (“Climbing Seven Summits”)
wapanda milima ni watu wenye moyo wa kufikia malengo na kufanikiwa
katika maisha yao.
Akiwa
Uingereza Moshi alipanda mlima wa Ben Nevis mrefu kuzidi nchi hii-
wenye mita 1,344 (futi 4, 409). Baada ya kuimudu milima mitatu sasa ,
Wilfred Moshi ameazimia kupanda milima katika mabara yote 7 duniani.
Anasema amebakisha milima mitano: Aconcagua ( Marekani ya Kusini ),
Kosciuszko (Australia), Vinson Massif ( Antarctica) McKinley(Alaska)
na Elbrus(Urusi).
Mungu ambariki Mtanzania huyu mwenye jazba na hamasa anayetuletea sifa
Story na CHUMA
No comments:
Post a Comment