Washiriki
wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012, walikamilisha zira yao ya
Kutembelea Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Manyara, Moshi na
Tanga kujionea vivutio vya utalii katika mikoa hiyo ambapo walimalizia
mkoani Tanga kwa kutmbelea Mapango ya Amboni mkuano humo.
Warembo
hao wakiwa katika mapango hayo ya kale waliweza kujionea vitu
mbalimbali ambavyo ni vya kipekee na vyakuvutia vilivyopo katika mapango
hayo ya asili ya zama za kale.
Miongoni
mwa vitu vilivyopo huko kwenye mapango hayo ni sanamu za aina
mbalimbali za Bikira Maria, Maandiko ya Quran, Daraja, sanamu za jinsia
ya kike na kiume, chui, na vitu vingine mbalimbali vya kuvutia.
Hapa
ni katika eneo ambalo linafananishwa na Mlima Kilimanjaro na hapa
warembo wakipanda mlima huo ndani ya Mapango ya asya Amboni mkoani
Tanga.
Hapa
warembo wakipiga picha katika kiti cha enzi. Ni jiwe lililochongeka
mithili ya sofa na ukiingia pangoni humo inapendeza kuchukua kumbukumbu.
Eneo hili ni linafananishwa na Mlango wa kupandia ndege na hapa warembo wakipanda na kutoka nje ya pango.
Bado pango hilo la Amboni linaendelea kukua. Na hapa warembo wakiangalia moja ya vitu vinavoota kila mwaka hasa wakati wa mvua.
Hapa huna budi kuinama na huko ndani waweza kuinuka bila kugusa juu.Wanapotokea..
Warembo wakiangalia moja ya vitu vya kuvutia na hapa waliangalia mchoro wa asili wa chui aliyelala baada ya kushiba.
Hakika
ukifanikiwa kupita hapa utapita pango zimana kujionea vitu vingi. Hapa
lazima utambae na wengi hushindwa kupenya hapa. Hata Father Kidevu
nilipenya na warembo walishangaa niliwezaje kupenya kirahisi.
Ni
full kushangaa kwa warembo hawa wa Redds Miss Tanzania 2012. Hakika ni
utalii wa ndani uliofanywa na warembo hawa lakini je ni watanzania
wangapi tunatalii katika maeneo ya utalii.
No comments:
Post a Comment