Mkurugenzi
wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa,
akihutubia kwenye Semina kuhusu Utalii, Tanzania. Semina ambayo
ilifanyika siku ya Jumamosi Tarehe 13 October 2012 katika mji wa
Redditch, nchini Uingereza. Semina ambayo ilihudhuriwa na Wataalam na
Wawakilishi mbalimbali kutoka katika sekta ya Utalii, iliyoandaliwa na
Britain Tanzania Society kwa kushirikiana na Redditch One World Link (ROWL), Uingereza.
Mkurugenzi,
Bwana Yusuf Kashangwa, akimkabidhi Mstahiki Meya wa Mji wa Redditch,
Bwana Allan Mason, zawadi kutoka Tanzania, kama heshima na kuthamini
mchango wa Ushirikiano mwema kati ya Mji wake wa Redditch na Tanzania.
Mstahiki Meya, Allan ameahidi kuetembelea Tanzania Mwakani.
Baadhi ya Wawakilishi katika Semina hiyo pichani, wakisikiliza kwa makini Mada mbalimbali zikitolewa kuhusu Utalii, Tanzania
Wawakilishi
kutoka sekta mbalimbali ya Utalii, waligawanywa kwenye makundi,
kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika kusaidia kukuza
na kuboresha Utalii Tanzania
Mkurugenzi
wa Kituo cha Biashara, London, Bwana Yusuf Kashangwa (kwanza kushoto),
akiwa kwenye Picha ya pamoja na Mstahiki Meya wa Mji wa Redditch, Bwana
Allan Mason, mara baada ya kumalizika kwa Semina hiyo. Wa kwanza kulia,
Bwana Mohamed, afisa kwenye Kituo cha Biashara, London.
---
Hayo
yalikuwa ni maoni ya wataalamu mbalimbali wa masuala ya utalii,
mazingira na maendeleo waliyoyatoa kwenye semina iliyoandaliwa mjini
Redditch kujadili Hali ya utalii nchini Tanzania.
Semina hii iliandaliwa kwa ushirikiano wa Redditch One World Link (ROWL) na Britain-Tanzania Society (BTS), ilifanyika
siku ya Jumamosi Terehe 13 October 2012, na mada kadhaa ziliwasilishwa
na kujadiliwa na wana semina wapatao 150 hivi. Mgeni rasmi katika semina
hiyo alikuwa ni Mstahiki Meya wa Mji wa Redditch, Bwana Allan Mason.
Mji
wa Redditch kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Redditch One World
Link (ROWL) una uhusiano wa kirafiki na mji wa Mtwara nchini Tanzania
tangu mwaka 1985.
Baada
ya hotuba ya makaribisho ya mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kituo cha
Biashara cha Tanzania Ubalozini London, alikuwa wa kwanza kuwaeleza wana
semina juu ya vivutio mbalimbali vilivyoko nchini Tanzania na pia juu
ya sera ya Utalii endelevu inayotekelezwa na serikali ya Tanzania.
Aligusia vipengele muhimu vya sera hiyo kuwa ni kuongeza mchango wake
katika pato la Taifa, kujali maslahi ya Taifa , ya watu wake, kuhifadhi
mazingira na rasilimali nyinginezo kupitia mikakati na mipango
mbalimbali na kusimamia utekelezaji wake na kwa kuwashirikisha wadau
wote bila ya kusahau wananchi wa kawaida kokote waliko katika maeneo
yenye vivutio asilia vya kitalii .
Watoa mada wengine walikuwa ni Bw. Nigel Nicoll, Mkurugenzi Mkuu wa African Travel and TourismAssociation (ATTA) aliyeongelea juu ya changamoto wanazokumbana nazo wadau wa utalii, Mark Watson, Mtendaji Mkuu wa Tourism Concern aliyeongelea
juu ya utalii, mazingira na kujali maadili. Bi Catherine Brenan
alielezea uzoefu alioupata baada ya kupanda mlima Kilimanjaro,
akichangisha fedha za kumalizia jengo la shule.
No comments:
Post a Comment