nmb

nmb

Thursday, December 27, 2012

MAKALA MAARUMU YA MAKUMBUSHO YA MJI WA BAGAMOYO


                                Tangazo hili lina jieleza kwa lugha ya kiswahili na kingereza
                          Eneo hili lina kumbukumbu za kihistori za dini ya kiislam,
Raia wa kigeni wakiingia kutalii kwenye majengo  hayo ya kale ya dini ya kiislam yaliopo kijiji cha Kaole wilaya ya Bagamoto mkoa wa pwani.
Leo ni taanza kukupa histori ya mbuyu huu ambao kwa mujibu wa muongozaji wa watalii ya ndani na nje ya nchi Bw Boniface Sangija '2 Pac' Mbuyu huu ambao uko kwenye kijiji hicho una umri wa miaka 500.
   Hii ni moja ya sehemu ya mbuyu huo
             Kibao hiki kimebandikwa katikati ya mbuyu huo

Mtandao huu uliwashuhudia watalii wa ndani na nje ya nchi wakipokea maelezo ya histori ya mbuyu huo kutoka kwa Bw Sangija kwenye T-shert ya njano jana.


KIJIJI cha Kaole kilichopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, ambacho imelezwa kwamba kalne ya 13 kilikuwa chini ya utawala wa wajemi kutoka nchi za kiarabu,sikuu hii ya Chris Mass kimefulika watalii wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania waliofika kushuhudia vitu vingi vya kihistoria vilivyopo kwenye kijiji hicho
.
Mtandao huu uliwashuhudia watalii hao  wakipokea maelezo ya histori ya mbuyu wenye umri wa miaka 500 kutoka kwa Bw Sangija mwenye T-shert ya njano jana.

Mbali ya Mbuyu huo watalii hao ambao watanzani ulipia gharama ya shilingi 1,000 na watalii wa nje hulipia gharama ya shilingi 20,000 walipata pia fulsa ya kutembela majengo ya kale yenye histolia ya kutisha,pamoja na kaburi la Bint Sharrifa Sharifu aliyekufa akiwa na umri wa miaka 13 ambapo kwenye kaburi lake kumejengwa jengo linalofanana na msikiti huku mbembeni kukiwa pia na makaburi ya watoto wachanga watatu 


Vile vile kwa upande wa dini ya kikristo pia kuna makumbusho na maajabu kwenye kanisani la Katoriki Parokia ya Moyo safi wa bikira Maria,kanisa hilo liko eneo la Misheni Bagamoyo,



Mtandao huu umefanikiwa kupata Picha na histori historia za mambo mbali ya kihistoria  kutoka kwa msimamiwa wa makumbusho hayo Bw Jastin Romani.



Mpendwa msomaji wetu Mtandao huu utaaza kukupa  picha  za histori kutoka Kijiji cha Kaole ambapo kila siku mtandao huu utarushwa tukio moja baada ya jingine.



Baada ya kukamilika kwa historia  ya kijiji cha Kaole ambayo itachukua takribani wiki moja,Makala hiyo itahamia upande wa pili wa makumbusho wa dini ya Kikristo,yaliopo pia mji huo wa Bagamoyo.


Makala hii itaendela kesho kwa kurusha hewani picha ya kisima chenye maji ya baraka ambacho kiko ndani ya msikiti wa kale .
    
NA DUNSTAN SHEKIDELE ALIYEKUWA BAGAMOYO

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis