nmb

nmb

Monday, January 14, 2013

Jay dee atangaza utalii wa ndani mlima Kilimanjaro



Msanii wa muziki Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee akiwa ameshikwa mikono kusaidiwa kushuka kutoka mlima Kilimanjaro aliko panda Jaanuary 8 mwaka huu na mumewe Gadner G Habash kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani.
Mhifadhi mkuu wa mlima Kilimanjaro Erastus Lufungulo akimuongoza msanii Lady Jay Dee mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro,shoto mwa Jay dee ni mpiga picha wa JayDee,Bw Justine Bayo.
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akimkabidhi cheti cha uthibitisho wa kufika kileleni msanii Lady Jay Dee.
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akimkabidhi Gadner Habash cheti cha uthibitisho wa kufika kileleni Gadner G Habash.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA), Erastus Lufungulo akimkabidhi cheti Bw. Justin Bayo baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Uhuru.
Msanii Lady Jay Dee,mumewe Gadner na mpiga picha wao Justine wakimsikiliza kwa makini mhifadhi mkuu wa Mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro(hayupo pichani).
Mume wa msanii Lady Jay Dee aliyekuwa ameambatana nae katika safari hiyo ya siku tano Gadner G Habash akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) mara baada ya kushuka katika lango kuu la Marangu.
Msanii Lady Jay dee akizungumza na wanahabari( hawapo pichani) mara baada ya kufanikiwa kushuka salama kutoka mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpoekea msanii Lady Jay Dee mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jay Dee, jana alifanikiwa kukamilisha ziara yake ya siku sita ya kupanda mlima Kilimanjaro, ikiwa na lengo la kutangaza mlima huo na kujionea upekee wa kivutio hicho.

Katika ziara hiyo iliyodhaminiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini (TANAPA), msanii huyo aliyeambatana na mumewe ambaye ndiye anesimamia kazi zake, Gadna Habash, waliwasili kwenye lango kuu la Marangu saa 12 jioni na kupokelewa na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA), Erastus Lufungulo.

Msafara wa Jay Dee ulianza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro Januari 8 na kufanikiwa kufika katika kilele chake chenye urefu wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kushuka mlimani, Jay Dee, alisema ziara hiyo imetoa mafunzo makubwa kwao na wakatoa wito kwa wasanii, waandishi wa habari na watangazaji nchini, kutembelea vivutio hivyo ili kufahamu yale wanayozungumza kuhusu hifadhi hizo.

“Ziara hii imenipa mwanga kama msanii, nimejifunza mengi na niwakumbushe tu wasanii wenzangu kuchukulia zoezi la kupanda la kupanda mlima Kilimanjaro kama moja ya majukumu na wajibu wao kama wananchi wa taifa hili,” alisema Jide.

Kwa upande wake mhifadhi wa KINAPA Lufungulo ametoa rai kwa wadau wote hasa wananchi wa kawaida kushiriki kupanda mlima huo, kwa lengo la kukuza utalii wa ndani.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis