Wizara ya Maliasili na Utalii imekusudia kurekebisha mipaka na ukubwa wa eneo la Pori Tengefu la Loliondo kutoka kilomita za mraba 4,000 hadi 1,500 ili kumaliza migogoro ya muda mrefu inayotoka na mwingiliano wa matumizi ya ardhi katika eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki amesema serikali imefikia uamuzi huo kama njia bora ya kumaliza tatizo hilo kiserikali.
“Ili kutatua migogoro iliyopo, kunusuru ikolojia ya Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro na pori Tengefu Loliondo, Serikali itameamua kutoa kilomita za mraba 2,500 kuwapa wananchi kuwa vijiji na wa kilometa za mraba 1,500 zitabaki serikalini na kuendelea kuwa na hadhi ya Pori Tengefu kwa ajili ya kulinda mazalia ya wanyamapori, mapito na vyanzo vya maji kwa ajili ya ustawi wa hifadhi na Taifa,’’ anasema Mhe. Kagasheki.
Mhe. Waziri aliongeza kuwa Serikali itawawezesha wananchi kuanzisha Jumuiya la Hifadhi ya Wanyamapori katika ardhi ya kijiji, na mipango ya matumizi Bora ya Ardhi ya vijiji katika eneo la Loliondo utaandaliwa na kuambatana na huduma za mifugo ndani ya vijiji.
Mhe. Kagasheki aliongeza kuwa Pori Tengefu la Loliondo ni eneo la serikali kisheria lakini baadhi ya vijiji wamelichukua na kulifanya kuwa lao na wengine wameingia mikataba na makampuni binafsi yanayofanya shughuli za uwindaji na utalii wa picha bila kufuata taratibu.
“Serikali imeona tatizo la ardhi kwa wanavijiji waliopo kwenye Pori Tengefu la Loliondo ndio maana limeamua kugawa eneo la ardhi kwao. Hata hivyo, nasisitiza sehemu ya vyanzo vya maji, mazalia ya wanyamapori na mapito ya wanyama katu serikali haitakubari kuwapa wananchi,” anasema Mhe. Kagasheki.
Mhe. Waziri anasema utekelezaji wa uamuzi huo unaanza mara moja kwa kushirikiana na Aidhana Wizara ya Mifugo itakayoandaa na ukubwa wa eneo la malisho lililopo katika kijiji pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kuona uhalali wa Kampuni zinazomiliki ardhi katika eneo lililohifadhiwa kwa madai kuwa wameuziwa na serikali za vijiji.
Aidha, Mhe. Kagasheki alisema, Serikali iko tayari kuangalia upya eneo kubwa lililotolewa kwa Ottelr Business Corporation ili kuona jinsi linavyoweza kupunguzwa ili wananchi wapate maeneo ya kufanyia shughuli zao na si kumfukuza mwekezaji huyo
No comments:
Post a Comment