nmb

nmb

Thursday, January 10, 2013

Wapiganaji wa majimaji,wakiwa na minyororo shingoni na miguuni,njaa,mateso,mauaji ya kikatili vyote hivyo katu havikuwatisha.

Wapiganaji wa majimaji,wakiwa na minyororo shingoni na miguuni,njaa,mateso,mauaji ya kikatili vyote hivyo katu havikuwatisha.

Mateso hayo ya kutisha waliyatafsiri kama wimbo mzuri wa kudai uhuru,walikuwa wazalendo wa kweli na upendo wa kimungu.

Hawakujali maumivu ya miili yao na hawakujali watapata nini ila kwa ajili ya kizazi cha watoto na wajukuu wao.

Inauma!! minyororo ile waliyofungwa shingoni na miguuni leo imefunga akili ya kizazi walichopigania na kufia.

Wanakata matawi waliyokalia,matunda yanaliwa na mti wake,mizizi inang'olewa na wanatema mbegu za matunda waliyokula juu ya majabali ya mawe na juu ya maji yenye kina kilefu.

Usiogope ukubwa wa mnyororo uliofunga shingo, mikono au miguu yako ogopa sana mnyororo unaofunga akili yako.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis