Hivi karibuni lens ya Camera ya Tembea Tanzania ilipata fursa ya
kutembelea Jiji la Mwanza na kuona maeneo mbalimbali ya jiji hilo. Picha
hizi zilipogwa pembezoni ya Ziwa victoria enao lijulikanalo kama Capri
Point. Mawe unayoyaona kwenye picha ya Juu ni miamba ijulikanayo kama
Bismark ambayo ni moja ya alama za jiji la Mwanza. kushoto ni Meli ya Mv
Victoria ikiwa imeegeshwa pembezoni ya Bandari ya abiria. Bandari kwa
ajili ya meli za mizigo ipo eneo jingine.
Jengo lenye maandishi ya Balimi ni Soko kuu la Samaki la Mwaloni aka mahakama ya Sato
Moja ya mtaa ukiwa unatokea Capri Point na kuingia mjini ambao umetunzwa vyema na ukatunzika.
Upande wa Ziwani nako kumepandwa majani vizuri na miti kadhaa.
Mlima huu niliambiwa unaitwa Mlima wa Kirumba.
Habari picha na KK
No comments:
Post a Comment