nmb

nmb

Sunday, February 17, 2013

Jua linapozama ndani ya camp site - Selous Game Reserve


Ni Picha zenye lengo la kukuletea machoni mwako mandhari ya tented campsite inavyokuwa mida ya usiku baada ya jua kuzama. hapa ni ndani ya pori la akiba la Selous na wageni hawa walilala kwenye mahema madogo waliyobeba wenyewe. Moto ni nyenzo muhimu sana kwenye tented camping kwani una kazi nyingi muhimu. kwanza kabisa hutumika kwa usalama ambapo wanyama wengi hupenda kukaa mbali ya moto hali ambayo inatoa uhakika wa usalama kwa kiwango fulani kwa wageni. mbali na hapo moto hutumika kutoa joto pale ambapo camp inakuwa imefanywa eneo lenye baridi baada ya jua kuzama. Mnapoenda tented camping kuni na vifaa vyote vya kupikia mnalazimika kuvibeba wenyewe.

 Kila mmoja huendelea na shughuli zake ktk kambi. Wapishi watakuwa bize kuandaa maakuli huku wageni nao wanaweza wakawa wamekaa mahali wakiongea na kufanya mrejesho wa yale walioyaona na kupanga ya kesho. yote haya yanakuwa yakiendelea chini ya mwanga wa mbalamwezi na moto wa kuota.



Shukran ya picha kwa mdau Rajab wa Wildness Safaris Tanzania

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis