Afande Sele
Mfalme wa Rhymes Tanzania, Afande Sele ameamua kufunguka
kufuatia migogoro inayoendelea kuibuka nchini juu ya imani za
kidini.
Afande amefunguka hayo jana jioni nilipokutana naye katika
studio za Diggital Vibes za mjini Morogoro, anapofanyia wimbo
wake mpya aliomshirikisha Belle 9.
" Ujumbe wa wimbo wangu mpya, unahusiana na maswala ya
imani za dini. Leo hii watanzania tumefik hatua ya watanzania
tumeanza kutengana kwa dini? aisee hii ni hatari, tunapoelekea
siko kabisa ndugu zangu, tunatengana, tunapigana, tunaharibiana
mali kisa imani ya dini wakati dini zimekuja na tulikuwa na
umoja na watanzania wote ni ndugu. nimekuja nawaletea ujumbe
na kila mmoja ausikie kupitia wimbo wangu mpya nimeimba na
Mdogo wangu Belle, lengu ni kuwahamasisha waanzania, tuziache
itikadi izo kwani mazala yake ni makubwa sana. tutajuta. wimbo"
Wimbo huwa wa Afande unazungumzia juu ya imani za kidini na
matukio yanayoendelea ivi sasa na Afande kiwahasa kuachana na
mambo hayo na tuishi kama ndugu kama zamani huku akizungumzia
hotuba ya hayati Mwl Nyerere.
No comments:
Post a Comment