Mwakilishi wa kampuni ya Tigo, Bw Joseph James akikabizi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi millioni kumi na sita (Tsh, 16,000,000) kwa wandaaji wa mashindano hayo taasisi ya
Zara Charity (Leila Ansell)
Tigo Tanzania kwa
kushirikiana na taasisi isiyo ya Kiserikali ya
ZARA Charity, taasisi tanzu ya kujitolea ya kampuni ya Utalii ya ZARA
Tanzania Adventures ambayo husaidia
shughuli mbalimbali za kijamii kwa kujitolea ndio waandaji Mbio hizo za za Sita
za Nusu marathon (kilomita 21.1) zijulikanazo kama ‘Tigo Ngorongoro nusu
Marathon’ zitakazofanyika kesho jumamosi ya Aprili 6, mwaka 2013.
Mashindano hayo ya mbio kwa mwaka huu yamebeba
ujumbe wa ‘Mbio za Mapambano dhidi ya Malaria’ yatafanyika katika mji mdogo wa
Karatu mkoani Arusha
Mnamo mwaka 2010, kampuni ya
Zara Tanzania adventures ilianzisha na kuwa mdhamini mkuu wa mbio za watoto za kilomita tano zilipewa jina
la ‘Ngorongoro Run: Kids’ Fun Run’, mbio ambazo zimetia chachu zaidi mbio hizo
za Ngorongoro Marathon.
Zaidi ya wakazi 5,000
wa Karatu wanashiriki na kuzifurahia sana mbio hizo ambapo pia hupata fursa ya
kujifunza masuala mbalimbali ya mapambano dhidi ya malaria.
Mbio
za Ngorongoro Marathon mwaka huu ni za kipekee sana kwani zinajumuisha
ushindanishaji wa makampuni mbalimbali ulioandaliwa na kampuni ya mtandao wa
simu za mkononi Tigo yatakayofanyika
kabla ya kuanza kwa mashindano hayo ambapo mshindi ataibuka na kitita cha dola
za kimarekani 20,000 ambazo atajitolea
kwa taasisi yeyote yenye uhitaji atakayoichagua.
Ufunguzi wa mbio hizo unatarajiwa
kuhudhuriwa na zaidi ya watu 3000 ambapo
Mgeni Rasmi atakayefungua mbio hizo anatarajiwa kuwa Naibu waziri wa Mali asili
na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.
No comments:
Post a Comment