Naibu wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na mwandishi wa mtandao huu |
Naibu wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amewataka viongozi wanaokalia mikataba ya wawekezaji katika sekta ya utalii nchini kufanya kazi zao kwa uadililifu na kwa muda muafaka kutofanya hivyo watachukuliwa hatua za haraka kwa kuwa nchi inahitaji wawekezeji wengi.
Kauli hiyo ilitolewa baada ya kuonekana kuna mapungufu mengi katika sekta ya utalii nchini kulinganisha na nchi za jirani hali ambayo juhudi za haraka zinahitajika kufika huko.
Naibu Waziri alisema kuna baadhi ya viongozi wenye dhamana ya kutoa nafasi kwa wawekezaji wanatumia nafasi zao kurudisha maendeleo nyuma kwa kushindwa kuwapa vibali wawekezaji hao mapema pasipo na sababu ya msingi.
Alisema endapo atagundulika kiongozi huyo atachukuliwa hatua za haraka kukomesha tatizo hilo kwa kuwa limeonekana sugu hasa kwa viongozi wa juu.
"Tunakwamishwa na matatizo mengi, likiwemo la baadhi ya viongozi kushindwa kutoa vibali kwa wawekezaji na kutumia nafasi zao kuwazungusha tunakemea jambo hilo na yoyote atakayepatikana atachukuliwa hatua" alsema mh Nyalandu.
Aliongeza kuwa kwa sasa sekta ya utalii nchini inatakiwa kupata wawekezaji wengi watakaofanya kazi na serikali katika kuinua sekta hiyo kwa kujenga hoteli za kitalii nyingi na kuitanga nchi kimataifa.
Alisema kupitia wizara hiyo inawataka viongozi na wakuu wa taasisi yeyote itakayoshindwa kutekeleza majukumu yake kwa hakika ataondolewa kazini na kushughulikiwa kwa kuwa anakwamisha maendelea ya serikali ambayo itatakiwa kuwaeleza wananchi walichokifanya kwa kipindi cha miaka hii mitano ya utawala wao.
Aidha naibu waziri huyo aliwataka viongozi wa hifadhi ya Ngorongoro kutoa maelezo sababu za wao kutokuwa washiriki katika mashindano ya mbio fupi za Ngorongoro zilizizofanyika.
"Walitakiwa kuwa sehemu ya mashindano haya, hakuna mwakilishi yoyote kutoka Ngorongoro, hili ni kosa wanatakiwa kujieleza hadi kufikia Jumamatu wawe wamewasilisha barua yao, kwa kuwa kulikuwa na ulazima wawepo haya ni mashindano yenye maana kubwa hapa Karatu" alisema Nyalandu.
Aliongeza kuwa kampuni binafsi inapojitokeza kusaidiana na serikali katika mapambano mbalimbali ikiwemo la maralia kama ilivyofanya kampuni ya utalii ya Zara Tanzania Adventures kwa kaundaa mashindano hayo yenye lengo la kupambana na ugonjwa wa malaria inatakiwa kuungwa mkono kwa karibu" alisema Nyalandu.
Nyalandu alikuwa mgeni rasmi katika mbio hizo zilizohamasisha utalii wa ndani pamoja na mapambano ya ugonjwa wa malaria, yalianzia kwenye geti kuu la Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na kumalizika Karatu, yaliandaliwa na kampuni ya Zara kupitia kitengo cha msaada cha Zara Charity.
No comments:
Post a Comment