nmb

nmb

Tuesday, April 16, 2013

FAHAMU JINSI YA KUTUMIA MAJI KAMA TIBA

MAJI ni dawa na ni kinga ya maradhi mengi. Kila mtu angekuwa anakunywa maji kama inavyotakiwa, kusingekuwa na maradhi kabisa. Huo ni ukweli wa tangu enzi za mababu zetu na umeshafanyiwa utafiti wa kutosha na kuthibitishwa na wanasayansi wengi duniani.


 
Ili upate faida ya maji kama tiba, ni lazima unywe maji mengi asubuhi kabla ya kuchomoza kwa jua na kabla hujapiga mswaki wala kula kitu chochote. Ujazo unaotakiwa kunywa ni kuanzia lita 1 na robo mpaka lita 1 na nusu, maji safi na salama na yasiwe ya baridi.

 Aidha, ukisha kunywa maji hayo usile wala usinywe kitu kingine hadi baada ya dakika 45 au saa moja, baada ya kupita muda huo, unaruhusiwa kupiga mswaki na kunywa au kula chochote utakacho na kinachokubalika kiafya (rejea makala zetu zilizopita). 


Kitu kingine cha kuzingatia ni kwamba baada ya kunywa maji, ni lazima uyanywe ndani ya kipindi cha dakika 5 au 10 tu na usifanye mazoezi hadi baada ya nusu saa. Wakati unafuata tiba hii kwa siku nzima, basi sharti liwe ukisha kula chakula, unywe maji kila baada ya saa 2 na ukae muda huo kabla hujala kitu kingine. 


Hata mtu asiye na maradhi yoyote, anashauriwa kunywa maji kwa mtindo huu ili kujikinga na maradhi katika maisha yake yote. Kwa wale wasiokuwa na uwezo wa kunywa kiasi hicho kwa siku zao za mwanzo, wanashauriwa kuanza na kiasi kidogo cha angalau glasi 2 na hatimaye wafikie 4. Usiogope wala usifikirie kutapika wakati ukinywa maji hayo, maji hayatapishi, bali dhana yako ndiyo inayoweza kukufaya utapike! 


Orodha ya magonjwa yanayoaminika kutibika, kuzuilika au kudhibitiwa kwa tiba hii ya maji ni pamoja na: Kisukari, shinikizo la damu, maumivu kwenye viungo (Joints Pain), matatizo ya moyo na kuzimia, homa ya uti wa mgongo (Meningitis), matatizo ya mkojo, kansa ya kizazi (Uterus Cancer), kikundu (hemorrhoid), matatizo ya tumbo, kuharisha, nyongo, kikohozi na chunusi.
Magonjwa mengine ni pamoja na kupooza mwili, athma, asidi tumboni, homa, kuumwa kichwa, upungufu wa damu (anemia), utipwatipwa (Obesity), kifua kikuu, magonjwa ya ini, matatizo ya hedhi, mataizo ya kukosa choo na magonjwa mengine mengi!


Iwapo watu wangeachana na unywaji wa pombe na soda, badala yake wakawa wanakunywa maji safi na salama kwa wingi, watafiti wa tiba ya maji wanaamini kwamba idadi ya wagonjwa hospitalini ingepungua kwa kiasi kikubwa sana duniani.
TIBA HII YA MAJI INAFANYA VIPI KAZI MWILINI?
MOSI: Unapokunywa lita moja na robo ya maji ndani ya dakika 5 au 10, baada ya kufunga kwa usiku mzima kwa muda usiopungua saa 8 hadi 10, shinikizo la maji yanayopita kwenye utumbo mdogo, huamsha na kuhuisha seli (cells) kwa haraka kuliko kawaida.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis