nmb

nmb

Friday, April 19, 2013

SIMULIZI: ASIA DIGITALI. SEHEMU YA 4




SIMULIZI: ASIA DIGITALI.
MTUNZI: George Iron

SEHEMU YA NNE

Siku iliyofuata majira ya saa moja jioni, Deniss alikuwa bize kubadili nguo, mara avae jeans.
“Ah hapa ataniona muhuni.”
Mara avae suti.
“Ah hapa nitaonekana mshamba sana….usiku huu na hili lisuti.”
Mara avae hiki mara kile.
Hatimaye akajituliza katika vazi la Jeans lakini juu akitua shati la mikono mirefu lililomkaa haswa.
Akaiendea gari yake na kuitia moto.
Safari ya kwenda kuonana na Asia.
Mtoto wa mjini.
Laiti kama angejua mtu anayekwenda kuonana naye.


Gari liliegeshwa katika maegesho ya magari kwa kulipia.
Deniss kabla ya kushuka katika gari lake, alichukua manukato makali na kujipulizia tena kisha akajitazama katika kioo.
Alikuwa ametakata.
Akatabasamu peke yake, ndevu zilizounda mfano wa ‘O’ kidevuni zikachanua. Akazidi kuvutia kumtazama.
Kwa utulivu na umakini wa hali ya juu akashusha mguu mmoja chini kisha ukafuata na ule wa pili.
Akabofya kitufe katika rimoti iliyobeba funguo za gari.
Yakatoka makelele kidogo yasiyokera masikioni.
Kisha akaanza kunyata akaufikia mlango, walinzi wakamkaribisha kwa macho, kisha wafanyakazi wa kike wakamlaki kwa bashasha.
Alifanania na mfalme.

Alipofika mapokezi alifuata maelekezo aliyopewa na Asia.
Simu ikapigwa katika chumba alichokuwa Asia.
“Samahani dada kuna mgeni wako hapa.” Sauti ya muhudumu ikatambaa.
Kimya kikatanda kisha akaitoa simu sikioni na kuuliza, “Unaitwa nani? Na je ulikuwa na miadi naye?” muhudumu alimuuliza deniss.
“Yah..nilikuwa na miadi naye…..naitwa Deniss..mwambie tuli…” kabla hajamalizia ngonjera zake muhudumu alikuwa amerejesha simu sikioni. Akatoa majibu.
“Nenda chumba namba 18…” alimweleza Deniss.
Japokuwa hakusema neno, Deniss alionyesha macho ya kuonyesha kuhitaji kuelekezwa zaidi. Muhudumu akaling’amua hilo.
Akamwita muhudumu mwingine akampa zoezi la kumpeleka Deniss kwa Asia.
Chumba namba kumi na nane.

Deniss akaugonga mlango.
Zikapita kama dakika tatu.
“Ingia…” sauti kutoka ndani ikajibu.
Deniss akakishusha kitasa akaingia.
Marashi yake yakasahaulika yalikuwa yananukiaje hapo awali.
Akakutana na marashi makali ya kisasa zaidi yakinukia kutoka ndani.
Akapiga hatua mbili, akakutana na mwanadada akiwa amejikita katika kompyuta mpakato (laptop) yake.
Alitumia dakika nyingine moja, akanyanyua kichwa. Akafanya tabasamu mwanana. Vishimo vikajichora katika mashavu yake.
“Hi Denny!!” sauti nyembamba kama inayojilazimisha kutoka lakini yenye kuliwaza na kusahaulisha kama kuna shida duniani ilitoka katika kinywa cha Asia.
Deniss akakodoa macho hakuwahi kuitwa kwa maringo namna hiyo hata mkewe a ndoa hakuwahi kumtolea sauti inayoliwaza namna ile.
“Hi!!” hatimaye alijibu.
“Karibu…karibu kitandani maana humu naona kuna kiti kimoja tu. Pole lakini next time nakukaribisha kwangu.” Alijieleza Asia.
Deniss akaketi.
Alichokosea ni kujionyesha kuwa mapema sana ameshangazwa na urembo wa Asia. Binti huyu alipata wasaa wa kumsoma.
Kosa kubwa sana wanalofanya wanaume wengi katika mfumo wa analojia.
Maongezi yakaendelea kidogo, asia akaitazama saa yake. Ilikuwa inakaribia saa mbili usiku.
Akaitwaa simu ya mezani. Akabofya namba kadhaa.
“Nahitaji mtu wa jikoni tafadhali.”
Simu ikakatwa.
Baada ya dakika tano. Hodi ikasikika.
Kwa mara ya kwanza Asia akasimama, kwenda kuufungua mlango ili muhudumu aweze kuingia.
Zilikuwa ni hatua sita tu lakini kila hatua haikutakiwa kuchezewa.
Kinguo kifupi alichovaa kiliruhusu michirizi ya utamu kuonekana nyuma ya goti, wepesi wake ukaruhusu mitikisiko ya kawaida na nyongeza ya mitikisiko ya kichina, mgongo nao haukuwa nyuma.
Asia alikuwa kifaa cha nguvu.
Akaufungua mlango. Muhudumu akaingia.
“Msikilize huyu kaka.” Asia alitoa amri kwa muhudumu.
Deniss akaanza kujiuma uma.
“Chipsi kuku….” Akaropoka.
“Mimi niletee mchemsho wa kuku.” Asia akauendea mkoba akaamua kulipa mapema. Akatoa kwa maksudi burungutu kubwa kiasi la pesa alizokuwa amezikomba katika akaunti yake.
Deniss akaziona.
“Mtoto hana njaa huyu.” Akabashiri.

Muhudumu alipoondoka, Deniss na Asia wakaendelea na stori za hapa na pale.
Mara simu ya Asia ikaita.
Akaitoa, akausoma ujumbe.
“Mh msichana mrembo kama wewe unatumia Nokia Obama ya tochi?” Deniss alitania.
Asia akafanya mfano wa tabasamu.
“Hebu simu yako…” akamuomba.
Deniss akamkabidhi, ilikuwa ni iPhone5.
“Umenunua bei gani hii?”
“Milioni moja na ushee.” Alijinadi Deniss.
Asia akatikisa kichwa kwa masikitiko.
“Deniss…..unajua kuwa kuna viwanja vinauzwa kijijini hiyo pesa uliyonunulia simu. Mimi niliyenunua kiwanja ambacho hakifutiki kabisa, na wewe uliyenunua simu nani amewekeza? Shtuka Deniss sisi ni vijana tunatakiwa kuwa na mawazo ya miaka kadhaa mbele sio kuwaza leo tu, chimbia pesa zako chini Deniss chimbia pesa kizazi chako kizikute, mwanao hataikuta hiyo sijui funifuni faivu sijui nini…simu uliyozungumza na mimi ndo hii je? Ulibaini tofauti?” asia alizungumza kwa hekima zote. Maneno kuntu kama kawaida yake. Yakamchoma Deniss akaanza kujichekesha kisha akajaribu kujibu hoja.
Asia alikisubiri kipengele hiki.
“Lakini Asia, huwezi jua mimi nimenunua kiwanja na bado nimenunua na simu, kama pesa ipo na inabaki nd’o ninunue viwanja tuuu.” Alijibu kwa kulalamika.
Asia akapata alichokuwa amehitaji.
“Kumbe bwege ana pesa chafu eeh…” alimuwazia huku akimtazama usoni.
Jicho la Asia likamwathiri kisaiokolojia Deniss lakini hakuweza kuanza.
Simu mfululizo zikawa zinaingia katika simu ya Asia.
Kila simu ilikuwa ya kibiashara.
Hakika Asia alikuwa namba nyingine. Deniss alikiri.

Majira ya saa tano usiku Deniss aliaga kuwa anaondoka.
Asia akamsindikiza mpaka mapokezi, wakaagana.
Deniss akatoweka bila kufanya lolote na Asia, alikiri kimoyomoyo kuwa alimuogopa sana binti yule mjasiriamali.

Siku iliyofuata mawasiliano yaliendelea kama kawaida.
Baada ya kutumia pesa nyingi kujaribu kumuweka sawa Deniss sasa Asia akaamua kulipua bomu lake.
Deniss akiwa anamuamini sana Asia kama rafiki wa karibu tena mshauri mzuri.
Ikafikia siku ambayo kamwe haitasahaulika katika kumbukumbu za Deniss.

Simu kutoka kwa Asia ilimkurupua kutoka katika kiti cha ofisi yake.
“Asia ametoka Msumbiji?” alijiuliza.
“Nambie.”
“Ukwapi Denny.”
“Ofisini vipi umerudi bongo?”
“Yeah nimerejea. Upo bize sana nahitaji kukuona.”
“Hapana sio bize sana.”
“Nipo huku Royal Temeke..kule pa siku ile.”
Dennis akaelewa akaingia garini akaelekea alipokuwa Asia.
Akamkuta chumbani akiwa mnyonge sana.
Tofauti kabisa na siku nyingine.
Vazi lake jepesi la kitambaa laini liliyaruhusu yale mapaja yaliyompagawisha Jumanne na hatimaye kulizwa gari yalikuwa nje.
Alikuwa amejilaza kihasara hasara haswaa.
Deniss alipoingia.
Asia hakushtuka akajiweka vyema kitandani huku akijifanya kujisitiri mapaja yake.
Deniss alitegemea Asia atasema jambo lolote, hakusema.
Akamsogelea pale kitandani.
Akamgusa.
“Asia…we Asia.”
Asia hakugeuka, Deniss akaamua kumgeuza.
Lahaula. Asia likuwa ameuchafua uso wake kwa machozi.
Mrembo alikuwa analia.
Kilio cha kimya kimya.
“Asia….kuna nini…nani Asia kakufanya hivi.” Deniss akataharuki.
“Niache Denny, niliumbiwa shida hizi. Niache tu.” Alizungumza huku analia.
Deniss hakukubali kumwacha. Akazidi kuuliza.
Ndipo Asia alipohamia digitali na kuendelea kucheza na akili ya Denny.
“Denny, mume wangu…mume wangu ananinyanyasa sana, mie wa kuwa naamua kulala hotelini kisa kitanda cha nyumbani kichungu.”
“Asia umeolewa?”
“Ndio. Lakini ni bure…bure kabisa Denny.”
“Nini kwani?”
“Ubunge wake ananiletea mimi hadi nyumbani….ubunge wake unanifanya mimi mtumwa. Ameona hiyo haitoshi kisa dini inaruhusu kaniongezea mke wa pili.” Asia alisikitisha na kama angekuwa muigizaji, wengi wangekuwa wanalia akiigiza vipande kama hivi.
Denny akahamaki, “kumbe Asia mke wa kigogo, ndo maana ana pesa huyu mtoto……dah…..watu wengine hawapendi shobo hata siku moja hajanambia.”
Denny akajaribu kumsihi sana asilie, Asia akazidi kulia.
“Denny asante kwa kuja katika maisha yangu, japokuwa ni karibia mwezi mmoja tu tangu tufahamiane nimejifunza mengi kwako. Na ukiwa kama rafiki mwema nimeamua kukuzawadia kitu kama utakuwa tayari.”
“Asante Asia hata mimi nafurahi kuwa rafiki yako. Nitafurahi kupata zawadi kutoka kwako” Denny alijibu huku mawazo yake yakiwaza ngono tu.
“Zawadi zipo za aina mbili, zote nitakupa.” Alisema Asia kisha akasita, “Zawadi ya kwanza itakuwa ni swali, na zawadi ya pili itaanza kabla ya zawadi ya kwanza.” Aliongea Asia huku akiwa ameremba sauti yake.
“Denny….nimeamua kujitolea pesa yangu milioni thelathini kwa ajili yako.”
“Kivipi?” aliuliza Denny.
“Nilikwambia huwa kamwe sinunui magari ya bei ghari wala simu. Nilikwambiaje?”
“Unachimbia chini..” alimalizia Denny.
“Ok..unapafahamu Bahari Beach..”
“Napafahamu kwa wazito kule….”
“Nataka nawe uwe mzito lakini kwa kujibu swali langu.”
“Niulize tu Asia.”
“Nitatoa katika akaunti yangu pesa taslimu milioni thelathini….nawe utatakiwa kufanya kitu kidogo tu milioni kumi….ifike milioni arobaini.”
“Ehee.”
“Kisha nakununulia kiwanja kikubwa pande zile, na ukionyesha uhai katika kujenga nitachota pesa nyingine nitakusaidia ujenzi….pesa inafukiwa chini mpenzi wangu….sio katika iPhone sijui nini” Asia alisema kwa maringo, walau aliweza kutabasamu.
“Nakufanyia haya yote kwa ukarimu ulionionesha kabla na baada ya kujuana.”
“Nilisema sihitaji jibu kwa sasa maana patakuwa na mjadala mrefu, kwa kuwa umezikubali zawadi zote, Denny ipokee zawadi yangu hii ya pili…”
Asia alimrukia Denny akamkumbatia, akajivika uso usiokuwa na soni hata kidogo. Akamnong’oneza Denny, “Ukiamua kuniona mimi Malaya sawa Denny lakini naomba niwe wazi…..Denny unanitesa…unanitesa Denny….”
Kijana hakukumbuka kama anayo pete ya ndoa, hakukumbuka kama anao watoto nyumbani.
Denny akachukua mkondo wa wanaume wengi, kuwa watumwa wa ngoni linapokuja suala la ana kwa ana na msichana.
Akamkumbatia Asia.
Ulikuwa mchezo wa dakika zisizopungua hamsini, sakafu ilihangaishwa, kitanda kiliteseka, bafu nalo liliona kilichotokea.
Deniss hakuwahi kufanyiwa manjonjo hayo na mkewe wa ndoa.
Walipotoka bafuni. Deniss akakumbuka kujibu swali.
“Nipo tayari kwa zawadi ya kwanza, nami nitakupa zawadi pia mpenzi.”
“Ok siku ukiipata hiyo pesa utanambia…” Asia akauliza swali la mitego.
“Sio kuipata ipo tayari..yaani siku ukiwa na nafasi tu my dear.” Deniss akajileta kwenye kumi na nane. Asia akachekelea maana hakuna mchezo alioupenda kama mchezo ndani ya kumi na nane.
“Basi tufanye kesho kutwa maana kesho nakimbia Mbeya…..narudi keshokutwa mchana…” alidanganya Asia ili aweze kujipanga kuchuma baada ya kupanda mwezi mzima.

***TEGO linakaribia kunasa……..nini kitajiri???

ITAENDELEA…..

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis