nmb

nmb

Sunday, April 6, 2014

Fisi akishiba lazima atafute kichaka au Tope...

Serengeti National Park - Tanzania
Tunamfahamu kama bwana afya, na hii ni kutokana na uwezo aliojaliwa Muumba wa kuweza kula mpaka mifupa. Wengi wetu hatufahamu gharama anayoipata fisi kutokana na kuwa na uwezo huo wa kula mifupa, kwato mpaka pembe za wanyama wengine. Ni kwamba, Mfumo wa mmeng'enyo wa fisi una tindikali ambazo ndizo zinampa kiburi mnyama huyu kupambana na mifupa iliyowashinda wenzie. tindikali hizi hufanya kazi ya kumeng'enya bidhaa zote ambazo Fisi huzitupiamo kinywani mwake. Zoezi la kumeng'enya mifupa na vyakula vingine huishia kuzalisha joto kali sana kwenye mwili wa fisi. Endapo fisi hatachukua hatua stahiki joto lile linaweza kupanda na kufikia viwango vya hatari vyenye kuweza kuhatarisha maisha yake. Joto huwa kali kiasi cha kuweza kuanza kuharibu baadhi ya viungo vyake vya ndani. 


Serengeti National Park - Tanzania
ili kuweza kukabiliana na joto hilo na pia kunusuru maisha yake, fisi hulazimika aidha kutafuta mahali ambapo kuna kivuli au Sehemu yenye maji au Tope. Sehemu hizi ndizo ambazo Fisi atazitumia kujaribu kupunguza makali ya joto ili lisimletee madhara zaidi. Chaguo la namna ya kujihifadhi hutegemea na mazingira aliyopo. Mathalani kwa fisi hawa tuliowakuta ndani ya Hifadhi ya Serengeti walilazimika kujitosa kwenye matope yaliyokuwa kandokando ya barabara ya Serengeti- Ngorongoro. hii ni kwasabu eneo ambalo tuliwakuta fisi hawa, hakukuwa na kichaka au mti wa kuweza kuwapa kivuli kizuri kupumzika. Hali hii hupelekea pia fisi kupenda kufanya mawindo yake usiku ambako hali ya joto huwa ni ya chini. Jua la mchana na shibe ni mateso kwa bwana afya. 

Serengeti National Park - Tanzania

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis