HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI
HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA
FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO
WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI
HUU NDIO MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE
WANANCHI MBALI MBALI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI
|
Mkuu wa mkoa Mbeya Abas Kandoro akiangalia ajali liyotokea mbalizi mbeya mchana wa leo
Watu 8
wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa akiwemo Mbunge wa viti
maalum Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa baada ya lory la mafuta kufeli
breki wakati likitelemka mlima wa Iwambi Mji wa Mbalizi na kuyagonga magari
matatu ambapo kati ya hayo magari mawili yaliteketea kwa moto .
Imeelezwa
kuwa ndani ya gari la Mbunge huyo kulikuwepo na watu wawili dereva wa gari hilo
aliyejeruhiwa miguuni na kichwani huku mwanamke mmoja anayesadikiwa
kuwa ni Katibu wa Mbunge huyo ambaye inadaiwa ameteketea kwa moto
na kubaki mifupa na majivu.
Ajali
hiyo ilitokea jana majira ya saa nane za mchana katika eneo la Mteremko
wa Iwambia mbapo alisema Lory hilo la mafuta likiwa na namba T81 4BTC na tela
lenye namba T815 BT linadaiwa kufeli breki na kuyagonga magari matatu likiwemo
gari la Mbunge huyo.
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya, Abass Kandoro, akizungumza na waandishi kwenye eneo la tukio
alisema ajali hiyo imesababishwa na magari manne ambapo kati yao matatu
yameteketea kwa moto papo hapo likiwemo gari la Mbunge Toyota Hilux.
Alisema,
gari lingine lililoteketea moto ni gari ndogo ya abiria Toyota Hiace
yenye namba T587 AHT ambalo lilikuwa na watu kumi ambao kati yao wapo
waliofariki na kujeruhiwana lory lenyewe la mafuta limeteketea kwa moto.
Akizungumzia
tukio hilo kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alisema baadhi
ya majeruhi wa ajali hiyo ni Mbunge Mary Mwanjelwa ambaye anaendelea kupatiwa
matibabu katika hospitali ya Teule ya Ifisi baada ya kuumia kwenye kiuno na
dereva wake ambaye ameumia miguu na kupata majeraha kichwani.
Majeruhi
wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali Teule ya Ifisi na
wengine hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na kwamba hali ya Mbunge inaendelea
vizuri.
Mtanzania,
lilizungumza na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo ambao walisema kuwa Lory hilo
la mafuta lilikuwa likishusha mlima huo wa Iwambi, huku mbele yake kulikuwa na
Lory lingine la mizigo mbapo dereva wa gari hiyo alifanikiwa kulipisha Lory
hilo na ndipo lilipoyagonga magari hayo mawili ambayo mbali na kupinduka
kandokando ya barabara pia yaliteketea kwa moto.
“Lory
la mafuta lilikuwa katika mwendokasi na ndipo lilipoligonga lory lingine la
mizigo na kisha kwenda kuyagonga magari madogo mawili na kusababisha
ajali hiyo kutokea,”alisema Alisi Mwakisapi.
Alisema,
Mbunge wa viti maalumu aliokolewa na bodaboda iliyokuwa karibu na eneo hilo kwa
kile alichokidai kuwa mara baada ya kufanikiwa kutoka ndani ya gari hilo dereva
huyo alimuona na kumchukua kwenye bodaboda na kumuwahisha hospitali.
“Katika
gari alilikuwa amepanda Mbunge, alikuwemo dereva na mwanamke mmoja ambaye
anadaiwa kuteketea kwa moto,”alisema
Hata hivyo, miili ya
marehemu tisa imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya na
hospitali Teule ya Ifisi majina yao hayajatambuliwa na kwamba mwili wa
mwanamke mmoja ambaye alikuwa kwenye gari ya Mbunge uliteketea kwa
moto.
|
No comments:
Post a Comment