Hii Ni Orodha Ya Makabila Ya Tanzania.
Kuna
matatizo kwenye majina kadhaa katika orodha hii, kwasababu mbalimbali.
Orodha hii inatokana na orodha ya Ethnologue ya lugha za Tanzania,
pamoja na tovuti nyingine. Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya
makabila ni majina ya lugha au lahaja badala ya makabila, na labda
majina mengine yaliandikwa vibaya. Juu ya hivyo, hakuna ufafanuzi wa
wazi kusema kwamba kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa
katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vinavyo
mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii
za aina tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa
vikundi tofauti kutokana na ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha
lugha zao.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani
katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila
yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani. Orodha hii
haizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi kutoka
vita katika nchi za jirani. Ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya
wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka
Arabia au Uhindi.
Waalagwa (pia wanaitwa Wasi),wanatokea Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa. Lugha yao ni Chasi. Waakiek,Waarusha,Waassa,
Wabembe ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kigoma, Wilaya ya Kigoma Vijijini. Lugha yao ni Kibembe.
Wabena ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Njombe.Lugha yao ni Kibena
Wabende ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Mpanda. Lugha yao ni Kibende,
Wabondei ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Tanga, karibu na Milima ya Usambara. Lugha yao ni Kibondei.
Wabungu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Chunya. Lugha yao ni Kibungu.
Waburunge ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa. Lugha yao ni Kiburunge
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu
wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani
Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo. Wachagga
wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine.
Kabila la kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo (ya
Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia
Mashariki Tarakea, Rombo hadi magharibi ya Kilimanjaro Siha, Machame.
Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Marangu, Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho,
na Wa-Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo,
Wa-Uru, na Wa-Siha.
Lugha ya Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka
unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo
Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kimarangu, Ki-Old
Moshi,Kikibosho, Kimachame, Kikirua na Kisiha. Lugha hizi zinakaribia
kufanana kulingana na jinsi makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano,
Ki-Old Moshi kinafanana na Kikirua, ambacho nacho kinafanana kidogo na
Kimarangu. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia
kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za
Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo
na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wamachame
ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.
Majina ya Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya
Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga
nchini Tanzania ni kama Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa,
Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo,
Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo.
Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Lamtey, Tairo,
Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi,
Urasa, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu. Rite, Makule, Minja,
Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo,
Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau,
Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.
Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni
kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba
Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni
Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa
kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu
zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za
kutafuta pesa kwa mwaka mzima.
Wadatooga (pia huitwa Wataturu, Wamang'ati au
Wabarabaig) ni kabila la Tanzania wanaoishi katika mikoa ya Manyara na
Singida. Lugha yao ni Kidatooga
Wadigo ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa
Tanga, hasa kwenye mji wa Tanga. Pia wako Kenya wanapoishi upande wa
Kusini wa mji wa Mombasa. Katika Kenya huhesabiwa kati ya mijikenda.
Lugha yao ni Kidigo.
Wadoe ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo. Lugha yao ni Kidoe.
Wafipa ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Rukwa, hasa katika wilaya za Sumbawanga na Nkansi. Lugha yao ni Kifipa.
Wagogo (mmojawao anaitwa Mgogo) ni kabila la Tanzania
ya kati, wenyeji wa mikoa ya Dodoma na Singida. Lugha yao ni Cigogo
(kwa Kiswahili hutamkika Kigogo).
Dini ya wengi wao ni Ukristo, hasa wa madhehebu ya Anglikana, halafu wa
Kanisa Katoliki. Historia ya Wagogo inaweza kuelezeka kwa kuangalia
yafuatayo: Utawala wa jadi, nyumba za asili, chakula kikuu na lafudhi ya
lugha. Majina ya ukoo ya Cigogo
majina hayo ni kama Mazengo, Cidosa, Cilongani, Malecela, Mwaluko,
Mavunde, Ndejembi, Manyesela, Mbogambi, Mdachi, Kapaya,Matonya, Mtunya,
Kusila, Nhonya,Mhalanyuka, Mbenaa, Chibile, Mdoli,
Lusinde,Njamasi,Majenda,Chiwamba,Mazoya,Ufinyu,Chilyawanhu,Magaya,
Ngoli,Chiwanga,Lubeleje,Makupila,Fukunyi
Waha ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kigoma, pia mpakani na Burundi. Lugha yao ni Kiha.
Wahaya ni Kabila linalopatikana katika Mkoa wa Kagera,
Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, kandokando mwa Ziwa Victoria. Lugha
yao ni Kihaya
Wahehe ni kabila la Tanzania ambalo kiasili linaishi katika wilaya za kaskazini za Mkoa wa Iringa, yaani Iringa, Kilolo na Mafinga.
Ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji. Ndiyo sababu wanazika wafu wao wakielekea mashariki.
Lugha yao (Kihehe) imegawanyika kiasi fulani katika lahaja (matamshi)
tofautitofauti kutokana na maeneo ambayo huzungumzwa. Inafanana
kimatamshi na kimaana na lugha ya Kibena iliyopo wilayani Njombe.
Wajita ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni Kijita.
Wakaguru ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilosa. Lugha yao ni Kikaguru.
Wakinga ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Makete. Lugha yao ni Kikinga
Wakuria ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara, pia wako Kenya. Lugha yao ni Kikuria
Waluguru ni kabila la Tanzania wanaoishi katika mikoa ya Morogoro na Pwani, hasa kwenye Milima ya Uluguru. Lugha yao ni Kiluguru.
Waluo
(pia Wajaluo) ni kabila hasa la Kenya. Wako pia Uganda ya msahriki na
wachache wanaishi nchini Tanzania katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni
Kiluo. Wenyewe hujiita Jaluo na lugha yao Dhulou.na mengi kuhusu
waluo.tembelea websitehii;www.jaluo.com utacheka mpaka ujambe
puuu.ongito nyamwanda 0784334032 en an jakiseru jakanyango
Waluo ni mkusanyiko wa kabila la kinilotiki ambalo
lilisafiri kutoka Afrika ya Kaskazini kufuata mto Nile kuja Kusini.
Waluo wengi wameenea kandokando ya Ziwa Viktoria kutokana na utamaduni
wao wa uvuvi. Kwa Afrika mashariki utawakuta nchini Sudan, Kenya, Uganda
na Tanzania.Waluo mashuhuri
• Gidi Gidi Maji Maji - Waimbaji wa hiphop
• Tom Mboya - mwanasiasa aliyeuawa 1969
• Barack Obama - mwanasiasa na seneta wa Marekani ni mwana wa baba Mluo
• Jaramogi Oginga Odinga - kiongozi wa Waluo wakati wa uhuru, mwanzilishaji wa chama cha KANU na makamu wa rais wa kwanza
• Raila Amolo Odinga - mwana wa Jaramogi na mwanasiasa muhimu wa kitaifa
• Robert Ouko - waziri wa mambo ya nje aliyeuawa 1990
Wamasai ni kabila wazawa wa Afrika la watu wahamaji katika wanaopatikana Kenya kaskazini Tanzania.
Wamachinga ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, wilaya za Kilwa na Lindi. Lugha yao ni Kimachinga.
Kwa kipindi cha karne ya 21 wamekuwa maarufu katika miji kwa kuuza bidhaa wakiwa wameshika mkononi wakisaka wateja.
Wamakonde ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mtwara. Pia wako Msumbiji. Lugha yao ni Kimakonde.
Wamwera ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, hasa kwenye Wilaya ya Nachingwea. Lugha yao ni Kimwera.
Wandengereko ni kabila la Tanzania wanaoishi katika
Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Rufiji. Lugha yao ni Kindengereko.Hapana,
Wandengereko hawaishi Mkoa wa Ruvuma bali mkoa wa Pwani kusini ya Dar es
salaam katika Wilaya za Mkuranga na Rufiji.
Wangindo ni kabila la Tanzania wanaoishi upande wa Kusini wa Tanzania. Lugha yao ni Kingindo,
Wanyakyusa (pia huitwa Wangonde au Wasochile) ni jina
kwa ajili ya watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za
kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania) upande wa kaskazini ya Ziwa Nyasa.
Lugha yao ni Kinyakyusa. Mara nyingi Wagonde upande wa kusini ya mto
Songwe nchini Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.
Kihistoria watu wanaoitwa leo Wanyakyusa waliitwa Wakonde na Wanyakyusa
walikuwa kabila kubwa kati yao. Wakati wa karne ya 20 "Wanyakyusa"
imekuwa jina la kundi kwa jumla. Hadi leo kanisa la kilutheri la KKKT
linatumia jina "dayosisi ya Konde" kwa eneo lake katika mkoa wa Mbeya.
Wakati Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini ya Ziwa Nyasa mwisho wa
karne ya 19 hawakuona tofauti ya kimsingi kati ya watu wa Malawi
kaskazini na wale wa sehemu za Rungwe wakawaita wote "Wakonde" kutokana
na jina lililokuwa kawaida ziwani.
Leo hii ni watu zaidi ya milioni wanaojumlishwa kwa jina hili, takriban
700,000 wanaokaa upande wa Tanzania na 300,000 wakikaa Malawi.
Wanyamwezi ni kabila la Tanzania wanaoishi katika mikoa ya Tabora na Shinyanga. Lugha yao ni Kinyamwezi.
Wasukuma ni kabila kubwa kutoka eneo la kusini na
mashariki ya Ziwa Viktoria, nchini Tanzania. Kabila hili hasa huishi
katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Mwaka 2001 idadi ya Wasukuma
ilikadiriwa kuwa 3,200,000 [1]. Lugha yao ni Kisukuma. Kisukuma ni
miongoni mwa lugha za Kibantu ambazo hubainishwa kama lugha mabishi.
Wayao ni kabila kutoka eneo la kusini ya Ziwa Nyasa.
Mwaka 2001 idadi ya Wayao ilikadiriwa kuwa 1,942,000, ambao 1,000,000
wanaishi Malawi, 450,000 ni wakazi wa Msumbiji, na 492,000 wako Tanzania
[1]. Lugha yao ni Kiyao.
Wazanaki ni kabila kutoka eneo la kaskazini-magharibi ya nchi ya Tanzaniai,
Wazaramo
ni kabila kutoka eneo baina ya Dar es Salaam na Bagamoyo, nchini
TanzaniaWazaramo ni sehemu ya Wabantu. Mababu wanaaminika waliingia
katika eneo la Tanzania katika milenia ya kwanza. Historia yao ya
kimdomo inasema ya kwamba walihamia pwani katika mazingira ya
Daressalaam kutoka Uluguru (Morogoro) katika karne ya 18.
Walipokaa kwenye pwani walikuwa karibu na makazi ya Waswahili wakaanza
kufaamiana na Uislamu. Taarifa za wakoloni Wajeruami mwanzoni wa karne
ya 20 zinaonyesha ya kwamba wakati ule Uislamu ulikuwa umeenea kati ya
Wazaramo na waliendelea kujiunga nayo haraka [2]. Siku hizi idadi kubwa
wa Wazaramo ni Waislamu.
Makabila Mengine Ni Haya Hapa Chini
Wakabwa,Wazigula,Wazinza,Wazyoba,Wahadzabe (pia wanaitwa
Watindiga),Wahangaza, Wakahe,Wakami,Wakara (pia wanaitwa
Waregi),Wakerewe,Wakimbu,Wasumbwa,Waswahili,Watemi(piawanaitwaWasonjo),Watongwe,Watumbuka,Wavidunda,Wavinza,Wawanda,Wawanji,Waware(inaaminikalughayaoimekufa),,Wanyanyembe,Wanyaturu(piawanaitwaWarimi),Wanyiha,Wapangwa,Wapare(piawanaitwaWasu),Wapimbwe,Wapogolo,Warangi(auWalangi),Warufiji,Warungi,Warungu(auWalungu),Warungwa,Warwa,Wasafwa,Wasagara,Wasandawe,Wasangu,Wasegeju,Washambaa,Washubi,Wasizaki,Wasuba,
Wanyambo,Wanyamwanga, ,Wandonde,Wangasa, ,Wandali,Wandamba,Wandendeule,
.Wangindo,Wangoni,Wangulu,Wangurimi (au Wangoreme),Wanilamba (au
Wanyiramba),Wanindi,Wamakua (au
Wamakhuwa),Wamakwe(piawanaitwaWamaraba),Wamalila,Wamambwe,Wamanda,Wamatengo,Wamatumbi,Wamaviha,Wambugwe,Wambunga,Wamosiro,Wampoto,Wamwanga,
,Wamagoma, ,Wakutu,Wakw'adza,Wakwavi,Wakwaya,Wakwere (pia wanaitwa
Wanghwele),Wakwifa,Walambya, Wakisankasa,Wakisi,Wakonongo, Wagorowa (pia
wanaitwa Wafiome),Wagweno, Waikizu,Waikoma,Wairaqw (pia wanaitwa
Wambulu),Waisanzu,Wajiji
1 comment:
Safi sana mkuu, Sasa tukumbushe na majina ya kiasili ya tanzania manake siku hizi wamejaa akina mohamed na akina john tu,aibu ya utakuta m2 majina yake yote matatu hamna hata moja la kinyumbani mfano, richard charles william, au hassan mohamed abdallah hii sini aibu? tupe majiana tuwa patie watoto wetu ili tulinde asili yetu TZ.
Post a Comment