HOTELI ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania, inathibitisha kufuru ya utajiri uliopo Tanzania.Singita
ndiyo hoteli nambari moja duniani, ikichukua tuzo hiyo kwa mwaka wa
pili mfululizo. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na taasisi maarufu ya
Marekani, US Travel + Leisure ambayo ‘hudili’ na viwango vya biashara ya
utalii duniani.Mmiliki wa hii Hotel ni mmarekani Paul Tudor ambae ameshawahi kuwekwa kwenye list ya
mabilionea katika jarida la Forbes na kwenye hii hoteli anashirikiana na
Luke Bailes wa Afrika Kusini
Sasakwa Lodge
hapa chumbani.
Hii ni moja ya Lodge inayojulikana kwa jina la Sasakwa Lodge iko kwenye kilima kinaitwa Sasakwa Hill.
Imejengwa kwa mawe na matofali, juu kwenye paa wameweka bati kisha
wakaweka mawe fulani yanapatikana maeneo hayo wao wanayaita "slates".hii yawezekana ndio Lodge kubwa kuliko zote Hotelini hapo ina vyumba vilivyojengwa kwa mtindo wa "cottages" vipatavyo 15 hivi.
Taarifa za uhakika ni kwamba kama wiki nne au tano zilizopita waigizaji
mastaa wa dunia Angelina Jolie na Brad Pitt walifunga ndoa ya siri na
yenye ulinzi kwenye hoteli hii ndani ya lodge ya Sasakwa, watu
hawakutakiwa kusogelea wala kamera hazikutakiwa.
Sabora Plains Tented Camp
Hii ni Sabora Plains Tented Camp, ambayo iko sehemu tambarare kama inavyoonekana kwenye picha. sehemu hii wageni wengi wanaofika hupenda kupumzika na kuota jua.
Miongoni mwa mastaa ambao mpaka sasa wameshafika kwenye hoteli hii ni
pamoja na tajiri wa dunia Bill Gates na baadhi ya washindi wa Olympic
2012
Marais
wa 42 na 43 nchini Marekani, Bill Clinton na George W. Bush, kwa
nyakati tofauti wamefikia kwenye hoteli hiyo baada ya kuvutiwa na sifa
zake zinazotikisa duniani.Bilionea
wa Kirusi anayemiliki Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich,alipotembelea nchini Septemba 2009, inaelezwa kwamba alilala kwenye
hoteli hiyo.Bilionea
wa Kihindi, Mukesh Ambani ambaye kwa sasa ni tajiri namba 19 duniani,
alifika nchini mwaka jana na kufikia kwenye hoteli hiyo.
Faru Faru Tented Camp ipo pembezoni mwa Mto Mara.
Angalia hema (tent) linavyoonekana kwa nje kisha angalia ndani
kulivyo kuzuri na mpangilio wake ulivyo wa hadhi ya "5 Star
Hotel.kiwango cha chini kabisa kulala kwa siku ni USD elfu moja na 50.
Asante sana mybrother "FARI" kwa picha
No comments:
Post a Comment