nmb

nmb

Wednesday, April 3, 2013

CHOMBEZO: ASIA DIGITALI SEHEMU YA KWANZA



CHOMBEZO: ASIA DIGITALI
 

MTUNZI: George Iron Mosenya
 

SEHEMU YA KWANZA.
 

Joto lililokuwa katika chumba kikubwa cha ‘internet café’ liliwafanya wateja wajipepee kwa kutumia makablasha kadhaa waliyoingia nayo ama kuyakuta katika chumba kile.Joto lile lilikuwa kero kwa kila mteja mle ndani, lakini kwa mtu mmoja tu n’do lilikuwa sherehe.Alikuwa ameyaona mawindo sahihi kabisa.Mawindo ambayo yangepewa ushirikiano mkubwa na lile joto.


Mkabala na mahali alipokuwa amekaa alitazamana na kijana wa makamo ambaye afya na mavazi yake pekee yaliidhinisha uwezo wa yeye kuwa ameegesha gari nzuri nje ya jingo lile na mfukoni hakukosa noti kadhaa zenye uzito wa kuitwa pesa. Jasho lilikuwa likimtiririka na alikuwa amejikita katika kujipangusa kwa kutumia leso yake.
 
Kabla umeme haujakatika kijana huyu alifanya siri na kuchungulia mapaja meupe ya binti huyu ambaye hakuteswa na joto lile bali ilikuwa sherehe. Wakati kijana huyu akidhani kuwa alichofanya kilikuwa siri sana…jicho kali na la kitapeli la binti yule liliweza kushuhudia matamanio ya kijana yule.


Sasa umeme ulikuwa umekatika, joto limetawala binti akaamua kuitumia nafasi.
“Atanijua mimi nd’o Asia.” Alijisemea wakati akifungua baadhi ya vishikizo vya blauzi yake. Alifanya hivi huku akkizuga kuwa anateswa sana na lile joto.Maziwa yake ambayo pia yalikuwa meupe pee yalionyesha mchirizi ambao asilimia kubwa ya wanaume wakiutazama hutamani kuona na kinachoendelea chini.


Asia hakuachia uhondo wote, alimuacha yule kijana katika mtihani wa matamanio.Kwa jicho lililofuzu kulaghai wanaume aliweza kuiona suruali ya kitambaa ya yule kijana ikitoka katika kutepeta na kukakamaa.Akafanya tabasamu la kusanifu, akijifanya anaitazama simu yake.Kijana wa watu hakujua kama anachezewa akili.“Kashajileta pumbavu zake.” Aliendelea kufanya tathmini.


Mara akaitupa karata ya mauaji ambayo aliamini kwa namna yoyote lazima yule mwanaume atajiingiza katika himaya yake.Asia kwa kutumia vidole vyake vyenye kucha bandia alibofya simu yake iliyokuwa katika mkoba.Ikaanza kuita akaichomoa. “Hellow……..mwenzangu….yaani najaribu kucheki Bro Smith, Skype umeme nao huko umekatika, nimemcheki kwenye simu, dah network ya Germany sijui vipi. Mbona yamenishuka mwenzako.” Asia aliongea kwa sauti nyororo inayobembeleza na bila shaka ilikuwa inatangaza maisha bora anayoishi kwani alikuwa katika kudeka.
 
Kimya kikatanda kama anayesikilizia kitu fulani kutoka upande wa pili. Kisha akafanya cheko, cheko lililoyaruhusu maziwa yake kifuani kucheza kidogo, akafanya kuiegemea simu akayarekebisha. Jicho lake kama kawaida likamchungulia muhusika wake.
Muhusika alikuwa amesahau kujipepea, alikuwa anatokwa jasho na alikuwa katika kushangaa.“Mi nataka kuondoka hapa, maana hakuna jipya, ..” akaweka kimya tena. Kisha akaendelea.“Naenda Msasani sahivi, lakini shoga mwenzio si unicheke kabisa mapema….sina gari hapa najishaua tu….maza kaenda nalo Mwanza, na mimi kuendesha ka Lexus kake sitaki.”Akaweka nukta tena.


“Mh…atoke wapi wa kunichukua wewe……naenda zangu kupanda daladala mie. Nitafanyaje sasa………baadaye basi Shosti.” Alimaliza maongezi akaufunga mkoba wake baada ya kuwa ameweka simu ndani yake.


Akasimama, akapiga hatua kadhaa, taratibu huku akiruhusu nyamanyama zilizovimbiana kwa nyuma na kumfanya apendeze zikitikisika kwa fujo. Yote haya yalitokea ili fulani aweze kuona.Macho hayana pazia, mikono ikamwenda kinywani, akakunja kunja sharubu zake, kisha mkono mmoja ukamponyoka na kuifikia suruali yake, akauingiza ndani na kusawazisha mambo.Macho ya Asia hayakukosea kumsoma, alikuwa ametamanika.

Kijana akasimama, akajifanya kunung’unika kutokana na huduma mbovu walizopata, hakukumbuka kudai pesa zake.Akapiga hatua kubwa akamfikia Asia.“Vipi dada na wewe wamekuchosha nini? Watu gani hawa yaani umeme umekatika hawawashi jenereta. Aaaargh.” Alilalamika.Asia akajichekesha kisha akasonya.“It’s boring…..yaani dah basi tu….but it sucks….” Akatema maneno, Kiswahili kwa mbali ung’eng’e mwingi.


Wakaendelea na mada ya kuwalalamikia watoa huduma hizo. Hadi wakaufikia ukumbi ule wa kuoneshana nani ni nani.Ilikuwa sehemu ya kuegeshea magari.“Kwani dada unaelekea wapi.” Kijana ambaye alikuwa hajajitambulisha jina akauliza.“Msasani, ngoja nikapate kero nyingine ya kugombania magari. We unaenda pande zipi au safari yetu moja?” aliuliza Asia huku akijua nini kinafuata.


“Mimi nafika Namanga hapo. Kuna watu naenda kuonana nao hivi mara moja. Dah hizi kazi hizi.” Alilalamika katika namna ya kujifagilia njia.“Poa kumbe gari moja twende ukanisaidie kuwania siti.”
 
Jamaa kusikia vile akajikoholesha kisha akamwonyesha Asia kwa kutumia kidole cha shahada, gari aina ya Noah nyeupe ikiwa imetulia ikimsubiri mmiliki. “Mwenzangu heri yako…poa kaka siku nyingine lakini hapa sirudi tena aisee.” Alisema Asia huku akiondoka.“Twende nikusindikize kidogo bwana..” alisihi yule kijana.
 
Asia akajifanya kufikiri kidogo kisha akauliza swali la kijinga.“Hamna mahali unapita maana mimi nina haraka kweli.”“Naenda moja kwa moja.”Asia akakubali, wakaongozana garini.Safari ya kuelekea Msasani.
 
Ndani ya gari maongezi ya hapa na pale yaliendelea….Asia kwa kutumia simu yake akafanya jambo jingine lililompelekea kujikuta anahamishiwa rasmi katika timu nzima ya digitali.Akaandika ujumbe baada ya dakika moja simu yake ikaita.


“Mh…sorry..simu yangu inatatizo la speaker I hope sitakuboa nikitumia loud.” Asia alisema huku akiyafinya macho yake katika namba ya kumhangaisha mwanaume dhaifu. “Aaah…hata usijali ongea tu….” Alijibu.Asia akapokea simu akaiweka katika spika kubwa.“Ehe nambie….” Akaanzisha maongezi. “Peter kanipigia mwenzangu…..”“Anataka nini?”
“Asia jamani…msamehe mwenzako …..kabembeleza sana ujue….” Sauti kutoka upande wa pili ikasihi.”


“Jackline, nakuheshimu sana…nakuomba kwa heshima ya urafiki wetu…usinambie lolote kuhusu huyo tapeli wa mapenzi, Jack umekuwa shahidi wa ujinga alionifanyia Peter….umeshuhudia uchafu wake wote…leo hii unamwombea msamaha…Jack kweli umenichoka kiasi hicho, amekulipa huyo Peter umwombee msamaha……ok Jack labda niseme neno moja tu….ulifurahia alichonifanyia sivyo…..Mbarikiwe sana “ Akamaliza huku analia, akaikata simu, uso ukiwa mwekundu, ngozi yake ya rangi ya chungwa ikikosa ustahimilivu na kuchafuliwa na machozi…kilikuwa kilio haswa. Asia alikuwa analia.


Kijana aliyekuwa anaendesha gari ambaye mwanzoni alikuwa amemtamani Asia alijikuta akipagawa, mara akaiegesha gari pembeni.Vioo vyeusi tii…nani atajua kinachoendelea ndani. Nd’o uzuri wa tinted Akaanza kumbembeleza Asia. Akamsihi sana asilie, Asia akawa analia huku anawalaani wanaume wote. Alimlaani Peter hadi yule kijana naye akamsaidia katika kumlaani.


“Mpendwe vipi nyie wanaume …mnataka roho zetu…mnataka tufe nd’o mjue kuwa mlipendwa au? Yaani mtalaaniwa nasema atalaaniwa huyo Peter, kwa chozi hili linalonitoka mimi Asia…Peter alitaka nini mimi nikamnyima, pesa zangu za kutumia chuo, pesa za kujaza gari mafuta zote nimempa mimi. Alitaka nini sasa, nimepigwa na dadiii mimi mamii akanichukia, kaka zangu wamenipiga makofi mimi. Kisa Peter, Peter….aah…” Asia aliendelea kulaani maneno yaliyomsulubu yule kijana.


Akiwa hajui cha kufanya Asia akiwa analia alimlalia, alimlalia kifuani, zile chuchu alizoziona kwa kuibia kule ‘internet café’ sasa zilikuwa zimemlalia zikimchoma katika namna ya kuleta hamasa, kucha za bandia za Asia zikalifinyafinya shingo lenye afya la yule kijana.


Pumzi za kupishana ndani na nje zikawa zinatesa katika sikio la yule kijana. Sasa alianza kupagawa. Huyu Asia alikuwa anajibembeleza ama.Akawa katika sintofahamu. Nani atampa jibu?Asia akalisikia paja lake likiguswa na kitu ambacho hakikuwepo hapo awali. Hakushtuka Akafanya tabasamu jepesi kisha akamzomea yule jamaa.Hicho kitu kilivimba kutoka katika suruali nyepesi.


“Bwege linawahi kweli kupata hamu hili.” Asia alikebehi kimya kimya.Hamu zikamzidi yule kijana, mara naye akakumbatia, mara akakumbatia kwa nguvu zaidi. Mara akaanza kunena katika lugha za maajabu zisizojulikana kitaifa wala kimataifa.


Mikono yake ilikuwa ikitalii katika mzigo wa titi mbili ndogo za Asia.Afadhali yeye alikuwa ananena kilugha.Asia alikuwa hoi kama aliyezirai.Jamaa akajua kuwa Asia kakolea.Laiti kama angejua kuwa Asia anatumia mbinu ya kidigitali, basi ni heri angebaki katika dunia ya analojia aliyokuwa anaishi awali.


“Baby…..Baby…..unaniua mweenzio….unaniaaa…..pliiz stop…..” “Am sore bebi…am sore vere sore….me you know…” Jamaa akajaribu kiingereza asichokijua, Asia akataka kupitiwa na kicheko.Akajikaza. Alikuwa kazini.


Mkono wa jamaa ukapenya katika mapaja…..Asia akajua jamaa anataka kumpima kina cha kisima na kutazama kama kina maji ama ni kikavu.“Bwege asije akanichafua bure..akavuka mipaka…..”Asia digitali akacheza kidigitali, alishagundua kuwa jamaa ni mwepesi sana.


Ulimi mkali kama ule wa kinyonga, ulimi ambao ulishausema uongo hadi uongo ukauzoea ukazama katika sikio la yule jamaa.“Uwiiiiiii….ooooohhh yeees..” jamaa akaganda kama roboti, mkono haukwenda mbele wala kurudi nyuma.Akazidi kunena kwa lugha zake zisizokuwa za kiroho.Asia akagundua kuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.Akafanya tekniki ya mwisho.Akajibandua katika mwili wa jamaa….akaanza kujifuta midomo, na kujifanya anaona aibu……jamaa kaduwaa tu hajui digitali inakwenda vipi. Analojia ilikuwa imemwathiri.
 
Jamaa akawa na aibu za kweli, suruali ilikuwa wima sana. Akajitazama, shughuli ikaja je airekebishe ama aicha ilivyo………

****Huyu ndiye Asia Digitali…….je historia yake inaanzia wapi…ni lini alihamia digitali…chanzo cha kuaicha analojia ni kipi???

****NI MWANZO TU WA CHOMBEZO HILI LA AINA YAKE AMBALO LINAKUWEKA KATIKA HALI MBILI, KICHEKO NA HISIA……..KAZI NI KWAKO…. ENDELEA KUTEMBELEA www.ngwesa.blogspot.com

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis