Sherehe
za kutangaza vivutio vya asili vya bara la Afrika zinategemea kufanyika
katika hoteli ya Mt Meru katika jiji la Arusha Tanzania tarehe 11
February 2013 kuanzia saa nane mchana.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania viongozi mbali mbali
wa kitaifa na kimataifa ambazo wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo
ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Mizengo Pinda. Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo
la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr Philip Imler
kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari kabisa
kutangaza vivutio Saba vya Asili vya bara la Afrika.
Tanzania
ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho
ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na wanyama
wanaohama wa Seregeti. Tanzania imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa
washindi ambao angalau kivutio kimoja ama zaidi Saba ya Asili Afrika.
Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.
No comments:
Post a Comment