Kwa wengi waliopata fursa ya kusafiri kati ya mikoa ya Iringa na
Morogoro watakuwa wanafahamu fika maeneo haya. Hapa ni geti ambalo lina
lengo la kumtahadharisha msafiri kuwa sasa anaingia eneo la hifadhi ya
Taifa ya Mikumi. Ni barabara yenye urefu wa takriban kilometa 50 ambazo
zinakatisha kwenye hii hifadhi.
Licha ya tahadhari na maelezo yote, matukio ya ajali za wanyama kugongwa
na uchafuzi wa mazingira ndani ya hifadhi unaofanywa na wasafiri
yanazidi kukithiri. Hali ya uchafu ndio inaonekana ki urahisi pembezoni
mwa barabara hii ambapo wasafiri wamekuwa wakitupa takataka bila kujali
ndani ya eneo la hifadhi. Hii si salama kwani inahatarisha maisha ya
wanyama. Makopo ya soda, chupa za maji ya kunywa zilizotumika sambamba
na alminium foil zilizofungiwa chakula zinaonekana kirahisi pembezoni
hususan mida ya jioni. Hali hii inahitaji juhudi za pamoja ili
kuwanusuru wanyama wanaohifadhiwa.
Hali unayoiona Mikumi ni tofauti sana na Hifadhi nyingine ambazo hazina
barabara zinazokatisha katikati. Wengi wa guides wanaopeleka wageni
kwenye hizi hifadhi huwa mstari wa mbele ktk kuwaelemisha wageni wao
kuhusu utunzaji wa mazingira na kuhakikisha kuwa wageni hao wanafuata
sheria na taratibu zilizowekwa ktk hifadhi husika. Kwa hili nawapongeza
waongoza wageni kwa kuwa mastari wa mbele kwenye utunzaji wa mazingira
na kuwalinda wanyama ndani ya hifadhi.
Uwepo wa hawa jamaa pembezoni mwa barabara hii na hata nje ya hifadhi
inatokana na kushamiri kwa vitendo vya utupwaji takataka ovyo
vinavyofanywa na wasafiri. kuanzia Mikumi mpaka Milima ya Iyovi na
Kitonga, hawa jamaa wanakuwa wengi hususan mida ya mchana wakisubiri
makombo yanayotupwa na wapita njia.
by KK
No comments:
Post a Comment