nmb

nmb

Friday, September 28, 2012

EPUKA KULA MISHIKAKI SEHEMU ISIYOELEWEKA,!!!!! ANGALIA HAPA

Ila kama we wa iringa poa tu
 
Epuka kula mishikaki kwenye migahawa isiyoeleweka,hiyo ni mitaa flani mateja wakichuna mbwa watengeneze mishikaki,....



  Bwana Rajabu akimchuna mbwa kama alivyokutwa.

Rajabu akimweka kwenye kiroba mbwa huyo tayari kwa safari.
 Rajabu akiwa kafungwa mikono baada ya kula kichapo.

Wananchi wakimpiga picha bwana Rajabu.

-Ilikuwa ni kwa ajili ya mishikaki, supu ya kuuza
UKISTAJABU ya Musa utaona ya firauni, hali hiyo iliwatokea wakazi wa Ubungo Kibangu pale mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Rajabu aliponaswa na wananchi akimchuna mbwa.Baada ya Rajabu kufumwa akifanya kitendo hicho, alipewa kibano na wananchi wenye hasira kali akakiri kwamba mbwa huyo alikuwa akimuandaa ili akamuuzee kama mishikaki na supu kwa wateja wake.

Baada ya wananchi kumtilia shaka anapopata nyama ya kuuza kutokana na hali yake ya kiuchumi kuwa duni, waliunda kikosi kazi cha kumchunguza ndipo arobaini yake ikatimia.

Mtoa habari huyo alisema baada ya wananchi kuchukizwa na kitendo hicho waliamua kumfikisha kijana huyo Kituo cha Polisi cha Kibangu. “Kijana huyo alipohojiwa na polisi alikiri kufanya biashara hiyo kwa muda mrefu,” kilisema chanzo chetu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alisema kuwa taarifa juu ya tukio hilo hajazipata na akaahidi kuzifuatilia na kusisitiza kuwa kama ni kweli kijana huyo alifanya kitendo hicho atachukuliwa hatua za kisheria.
Stori na  globalpublisher

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis