nmb

nmb

Sunday, September 16, 2012

Karibu moro tuishi kama Culture


 Nani kasema ndizi ni kwa Bukoba, Kilimanjaro na Mbeya pekee? hapa ni Madizini Morogoro wanasema nao Moro wanalima ndizi

Kwa wenyeji wa Morogoro kawaida ndizi huliwa zikiwa mbivu au kama vitafunwa (kwa kunywea na chai). Huwezi ukapikiwa ndizi halafua ukasema kuwa leo nimekula chakula. Hata kama watachanganya na nyama bado ni vitafunwa tu. Chakula cha heshima kwetu ni wali! Angalia hii mikungu ya ndizi
  
Ndizi tamu kutoka Morogoro. Msichana mrembo akiziweka sawa
 
Mfanyabiashara wa ndizi katika kijiji cha Magole wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Fadhil Seleman akikokota baiskeli iliyosheheni mikungu ya ndizi baada ya kununua shambani kisha kuuza kwa wenye m,angeni kijijini hapo kwa bei ya jumla ya sh 2,000 hadi sh 2,500.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis