nmb

nmb

Sunday, September 30, 2012

CHEKI TAMASHA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO LILIVYOKUA


 mtoto mwenye umri wa miaka 4 Nyambuli Mganga akiwa na kikundi cha sanaa na utamaduni  kijulikanacho kwa jina la Utandawazi Theatre Group Matwigha  Chalo kutoka Nansole Ukerewe akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Ukerewe inayojulikana kwa  jina la Obusimbula  katika meza kuu ,ambaye amekuwa kivutio  kutokana na kucheza kwake mwenyewe bila kuelelezwa wakati maonesho ya 31 ya Tamasha na Sanaa na Utamaduni liliyofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni(TAsuBA) iliyopo Bagamoyo, mkoa wa Pwani ,. Nyambuli ambaye anarithi utamaduni huo kutoka kwa mama yake, Wiliherimina Kebela . Maonesho hayo yamaeambatana  na Sherehe za mahafali ya 23 ya  taasisi hiyo zilizofanyika  jana(juzi).

Baadhi ya wahitimu wa Stashahada ya Juu ya Sanaa na Utamaduni wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasm Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya  Mwenyekiti  wa Bodi ya  Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na   Utamaduni(TaSuBa), Profesa Elias Jengo(kushoto) ambaye ni Mhadhili  wa taaluma hiyo katika Chuo Kikuu cha Dares Salaam(UDSM)i,  aliyeko katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya  Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Vijana, Profesa Hermas Mwansoko na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Juma Bakari.Wengine ni baadhi ya wakufunzi
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya  Mwenyekiti  wa Bodi ya  Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na   Utamaduni(TaSuBa), Profesa Elias Jengo ambaye ni Mhadhili  wa taaluma hiyo katika Chuo Kikuu cha Dares Salaam(UDSM),akimpatia cheti mhitimu wa Stashada ya Sanaa na Utamaduni , Charles Kiswaga katika mahafali ya 23 ya yaliyofanyika kwenye ukumbi wa maonesho chuoni hapo. Katikati Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Juma Bakari  na kulia ni  Mkuu wa  Idara ya Taaluma  Michael Kadinde
  Stori na Blog za mikoa Pwani yetu

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis